Blogger Widgets

September 11, 2013

Huyu Ndio Mwanafunzi aliyezaa Mtoto Huyu Na Diamond Platnum.NA HII Ndio Skendo Nzima Jinsi Ilivyokuwa





Video: Shasha akiongea na GPL kuhusu kuzaa na Diamond.
MREMBO Sasha Juma, 20, kwa sasa anapitia kipindi cha majuto, analipia gharama ya kujivalisha ubandidu na kujisingizia kupewa mimba na supastaa, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
Sasha, akiwa na macho makavu, alitamka mbele ya waandishi wetu kuwa mimba hiyo aliyopewa na Diamond, ilimgharimu kufukuzwa shule akiwa kidato cha nne mwaka jana.
Unadhani Sasha analo tena? Ameshaumbuka na baada ya simulizi yake ya kutunga kushtukiwa, hivi sasa mrembo huyo anatishia kujiua.
Mr. Juma ambaye ni baba mzazi wa Sasha, aliliambia  “Huyu mtoto ametishia kujiua, anajua makosa aliyoyafanya. Anataka kutuvuruga vichwa, ukweli ni kwamba kila alichokisema kuhusu Diamond ni uongo mtupu.
“Nahisi kuna mtu yupo nyuma yake, sasa anataka kumtumia ili kumchafua Diamond, upande mwingine akili yangu inaniambia yule mtoto anataka umaarufu, maana najua yule ni mwigizaji, sasa pengine anataka kutoka.”

UONGO WA SASHA
Tulipata taarifa kuhusu malalamiko ya Sasha ambaye alikuwa akidai kupotezewa dira ya maisha na Diamond kwa sababu alimpa mimba na kumtelekeza na mtoto mwenye umri wa miezi minne.
Baada ya kupata ‘tipu’ hiyo, mwandishi wetu alimsaka kwa udi na uvumba mpaka Septemba 4, mwaka huu (Jumatano ya wiki iliyopita) ambapo mrembo huyo alitia maguu kwenye mjengoni.
Baada ya kuwasili makao makuu , Bamaga, Mwenge, Dar es Salaam, Sasha aliingizwa kwenye chumba maalum chenye mitambo ya kurekodi sauti na picha kisha akaanza kumwaga simulizi yake.
Alidai kuwa alikutana na Diamond, Mlimani City, mwaka jana, wakapeana namba za simu kabla ya kuanzisha uhusiano wa kimapenzi ambao uliwafikisha kwenye ‘kategori’ ya kuparamia kitandani na kutenda mchezo wa baba na mama pasipo kutumia na kinga.
“Nilipopata mimba Diamond alinishawishi nisitoe, akaniahidi atanisomesha hata kama nitafukuzwa shule. Baadaye nilifukuzwa shule, akazidi kunipa moyo kwamba atanilinda. Mimba ilipokuwa kubwa akapotea, nilipozaa hakujitokeza.
“Diamond akawa siyo yule ambaye alikuwa ananipa moyo. Alibadilika, hali hiyo ikanifanya nione mwanangu hana baba, hata cheti za kuzaliwa, sijamwandika Diamond, mtoto wangu nimempa ubini wa baba yangu, yaani ya Juma.”

NI UONGO MTAKATIFU
Ili kukamilisha habari hiyo ambayo ilitoka kwenye gazeti hili, toleo la Jumamosi iliyopita, mwandishi wetu aliwasiliana na baba mzazi wa Sasha (Mr. Juma) ambaye alipoambiwa kuhusu mwanaye kuzaa na Diamond, alishtuka kisha akasema:
“Unajua yule mtoto sikai naye, anaishi na mama yake. Mimi sijui chochote ila nashangaa, inawezekanaje apate mimba mpaka azae mimi baba yake sijui? Ngoja niongee na mama yake.”
Mr. Juma alipiga simu kuzungumza na mama yake Sasha mbele ya mwandishi wetu. Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo;
MR. JUMA: Habari yako.
MAMA SASHA: Salama tu, za kwako?
MR. JUMA: Namshukuru Mungu, ebwana mbona Sasha kaongea na mwandishi wa habari anasema kapewa mimba na Diamond na amezaa?
MAMA SASHA: Wewe si unajua haya mambo ya vijana?
MR. JUMA: Mambo ya vijana kivipi? Ina maana mtoto anapata ujauzito mpaka anazaa wewe na baba yake hamjui?
MAMA SASHA: Baba nani, si wewe?
MR. JUMA: Mimi baba yake sijui, ndiyo maana nakuuliza wewe, maana nimesikia umekuwa unawasiliana na Diamond kuhusu hili.
MAMA SASHA: Nani kakwambia? Nimeshasema hayo ni mambo ya watoto, naomba umuulize mwanao vizuri, kama hauna namba yake nikutumie.
Katika mazungumzo hayo, Mama Sasha, hakumpa majibu ya moja kwa moja mzazi mwenzake, kuhusu binti huyo kupata mimba, kuzaa na Diamond kuwa mhusika.

RIPOTI YA WIKI HII
Mr. Juma alifika ofisi za Global Publishers na kueleza: “Jana (Jumapili iliyopita), nilimchukua Sasha na kuzungumza naye kwa kirefu, kwa kifupi alikiri kuwa hajawahi kupata mimba na yule mtoto si wa kwake.
“Mtoto imebainika ni wa dada yake, yaani mtoto mkubwa wa Mama Sasha ambaye anaitwa Khadija. Kuna kitu cha kujifunza hapa kuwa Sasha aliwadanganya mpaka watu ambao niliwakabidhi ili wamsaidie kisanii.
“Kabla sijaongea kwa kirefu na Sasha, nilizungumza na Thabit Abdul (mwanamuziki wa Five Stars) ambaye nilimkabidhi kwake kumsimamia kisanii, nikamuuliza inakuwaje mtoto anapata mimba? Akanijibu hata yeye anashangaa. Kwani hata yeye alishangaa kumuona Sasha akiwa na picha nyingi amebeba mtoto kwenye simu yake.
“Akamuuliza umezaa akajibu ndiyo. Hisia zangu zinazunguka katika mambo mawili, ama aliamua kutunga ili kupata umaarufu kupitia jina la Diamond au alitumwa na mtu. Jana wakati nazungumza na Sasha, nilikasirika sana, nikaona hatutafika pazuri.
“Ikabidi nimpigie simu rafiki yangu mmoja ili amwite azungumze naye. Kweli alimwita wakazungumza, baadaye yule rafiki yangu akaniambia Sasha kasema anaona mambo yanazidi kuwa makubwa, kwa hiyo anataka kunywa sumu afe. Namshangaa sana huyu mtoto, sijui ana kichaa gani?”

UKWELI NI HUU
Kwa mujibu uchunguzi wetu usio na shaka, mtoto aliyepigwa picha akiwa amebebwa na Sasha, mama yake halisi ni dada wa mrembo huyo ambaye ni Khadija.
Sasha na Khadija wanaunganishwa na mama yao lakini kila mmoja ana baba yake.
Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa kwa sasa Khadija anaishi na mwanaye mkoani Tanga, huku Sasha akiendelea kupuyanga ndani ya Jiji la Dar, akiwa hajui tamu wala chungu ya kunyonyesha, vilevile hajawahi kusikia uchungu wa uzazi wala hatambui sura ya ‘leba’ ilivyo.
Khadija akizungumza kupitia simu ya Mr. Juma, huku mwandishi wetu akifuatilia mazungumzo, alisema: “Nikija Dar nitafika Global, mimi ndiyo mama wa yule mtoto na zile picha Sasha alipiga na mtoto siku ya arobaini yake.
“Sasha anataka kunisababishia matatizo na baba mzazi wa mtoto. Mimi kama mama mzazi wa mtoto, simjui Diamond, kwa hiyo hahusiki chochote na mtoto wangu.”
Aidha, Mr. Juma alisema kuwa alimpigia simu Diamond na kumuweka sawa kuhusiana na tuhuma ambazo binti yake alimsakizia.
“Diamond anajua kila kitu, nimeshaongea naye na nimejaribu kumtaka atulize munkari, maana ni wazi zile taarifa zimemchukiza sana. Kweli zimemchukiza.”

DIAMOND ANASEMAJE?
Gazeti hili lilipozungumza na Diamond, alisema: “Nilishasema simjui huyo Sasha, ahadi yangu ipo palepale, nitampeleka mahakamani. Amenichafua sana.
“Masharti yangu ni haya, kama anataka nimsamehe aende kweye redio na televisheni akatangaze kwamba sijampa mimba.”

ONYO
Aibu ambayo Sasha anakutana nayo sasa na tishio la kuburuzwa mahakamani ambalo analikabili kutoka kwa Diamond ni onyo kwa watu wengine ambao wamekuwa na tabia za kuwasingizia wenzao ili kujipatia umaarufu.

No comments:

Post a Comment