Blogger Widgets

September 5, 2013

Utata Ulikuja ni Jinsi Huyu Kahaba alivyokutwa akaiwa anajiuza Karibu na Msikiti

Kahaba  mmoja   alijikuta akiambulia kichapo kikali toka kwa vijana wa kiislamu baada ya kunaswa akijiuza karibu na msikiti wao..

Wakati mwanamke huyo akicharazwa bakora, nguo ya ndani ilimvuka huku akipiga kelele kuwa hatarudia kufanya hivyo na kama akirudia basi akatwe kichwa.

Kutokana na kukerwa na vitendo hivyo, vijana hao wanaofanya ibada katika msikiti huo, waliamua  kuwatafuta vijana wa ulinzi shirikishi na kuwapa kazi hiyo ya kuwakamata na kuwacharaza bakora kisha kuwapeleka katika kituo hicho cha polisi.


“Tumeamua kuwakamata na kuwacharaza bakora, hawana ustaarabu wala busara hawa, wanakojoa na kutupa kondomu  hovyo, “ alisikika mmoja wa vijana hao.
Mmoja wa vijana hao aliyekuwa akisimamia kwa karibu zoezi hilo, aliwaambia waandishi wetu kuwa wameamua kufanya hivyo na litakuwa zoezi endelevu kutokana na wanawake hao kutokuwa wasikivu kwani kila wanapoambiwa juu ya kukaa mbali na nyumba hiyo ya ibada hawasikii.

Alisema kuwa siku moja wanawake hao walimtoa udhu muumini mmoja ambaye alikuwa akienda kuswali alfajiri baada ya kumshika na kusababisha akose kuhudhuria swala siku hiyo.


Hata hivyo, wakati mahojiano yanaendelea, mmoja wa askari waliokuwa zamu aliamuru mwanamke huyo aingizwe lokapu kusubiri kesho yake aunganishwe na wenzake kisha wapelekwe mahakamani.

Habari zilizotufikia  ni kwamba baada ya kufikishwa mahakamani na kukutwa na kosa la uzururaji, wakahukumiwa kifungo cha miezi sita jela au faini ya shilingi elfu hamsini ambapo walilipa kiasi hicho na bado wanaendelea na biashara hiyo maeneo hayo.