Blogger Widgets

November 2, 2013

Bob Junior na Ashaley toto,Mtoto Mzuri wa Kenya wafunguka Juu ya Uhusiano wao Ulisababisha Bob Junior Kuachana na Mke wake

 
 
  Bob Junior na Ashley

Mwanamuziki maarufu wa Bongofleva Bob Junior amekana habari zilizoanza kusambaa mitandaoni kuwa yupo kwenye dimbwi la mapenzi na Ashley Toto ambaye ni muigizaji wa filamu za Kiswahili kutoka Kenya lakini akiwa na makazi yake nchini Ujerumani, Ashley pia ni promota wa muziki na amekuwa akifanya kazi na wasanii mbalimbali wa Afrika mashariki kwa kuwapeleka ujerumani kufanya shows na kwasasa yupo Kenya. Habari ni kuwa hata ndoa ya Bob Junior imevunjika kisa kikiwa ni wawili hao kujinafasi kwa raha zao. Baada ya habari hizo kuanza kuenea na kufika hapa Swahiliworldplanet ilibidi kuwatafuta wasanii hao wawili ili kuwauliza kuhusu issue hiyo na wa kwanza kupatikana alikuwa ni Ashley ambaye alitumiwa ujumbe juzi kuhusu kuwa mapenzini na Bob Junior na alijibu kwa ufupi "sijui lolote samahani" na alipobanwa zaidi alisema "sisi sio wapenzi we are just friends ....more information muulize mwenyewe"

Baada ya hapo ilibidi kumgeukia Bob Junior na kumtumia ujumbe jana ila leo akajibu ujumbe huo kwa kusema "
hapana si kweli, hata blog iliyotoa habari hiyo inaitwa Udaku blog so nadhani ushajua hakuna ukweli"Swahiliworldplanet ilipomuuliza kwa hiyo upo na mkeo Halima(ambaye ni muigizaji wa filamu) kama zamani hamna tatizo lolote alijibu kwa kusema "kwa sasa sina mke kaka nipo single"