Blogger Widgets

November 18, 2013

Mambo Yabadilika Kati ya Ray Kigosi,Mainda na Johari.NI AIBU


KIMENUKA! Kambi mbili za wasanii wanaotamba katika tasnia ya filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ na Blandina Chagula ‘Johari’, zimetupiana matusi mazito,

Chanzo cha yote ni Mainda kufunguka juu ya uhusiano wake na ‘kaka mkubwa’ katika tasnia ya filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na kufichua jinsi Johari na msanii mwingine, Chuchu Hans walivyomuingilia katika penzi hilo.
Mainda alimwaga ‘upupu’ huo katika Gazeti la Risasi Mchanganyiko Jumatano iliyopita na kumfanya kila shabiki wao awashwe na habari hiyo.


Blandina Chagula ‘Johari’.
SIKIA KEJELI ZA JOHARI
Mara baada ya kutoka kwa habari hiyo, Johari alinukuliwa na gazeti moja (siyo la Global Publishers) akisema kwamba Mainda amembipu, atampigia akiashiria kwamba atajibu mashambulizi hayo.
Hata kabla ya kufanya hivyo, Johari aliwaambia waandishi wetu kwamba Mainda amewavua nguo na kuwaweka hadharani.
TIMU JOHARI
Kwa upande mwingine, baadhi ya wasanii wakubwa wanaoitumikia Kampuni ya Ray na Johari (RJ), kurekodi kazi zao, (Team Johari) wakamshambulia Mainda kwa matusi mazito kupitia mitandao ya kijamii kama vile Instagram na BBM.

 
Vincent Kigosi ‘Ray’.
MATUSI MAZITO
Mbali na kutumia njia ya mitandao, baadhi ya wasanii hao walidiriki hata kumpigia simu Mainda na kumnanga ‘laivu’.
MAINDA AJIBU MAPIGO
Akiwa bado hajapoa moto wa kile alichokidhamiria kukiweka hadharani, Mainda au Smallbaby kama anavyojiita, alijibu mapigo hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiungwa mkono na timu yake (Team Mainda).
Kwanza Mainda aliandika katika mtandao huo kuwaonya wale wanaunda makundi kumtukana kisha akasema kuwa haogopi kutukanwa kwani ameshatukanwa tangu akiwa tumboni kwa mama yake.
Mainda aliandika kwamba yeye hajawavua nguo akina Johari na Chuchu bali wamejivua nguo wenyewe kwa kufikia hatua ya kugombea ‘shingo’ (Ray).
Kama vile haitoshi, Mainda alidiriki kumwita Johari kwa jina la Jini la Shinyanga na kumwambia kuwa yeye siye mpinzani wake, kwani hawezi kugombea mwanaume ndiyo maana amemtupilia mbali.
Ray naye alijibu mapigo hayo kwa kuandika: “Siri ya mchezo naijua mimi…” Jambo hilo lilizua maswali mengi kwa watu waliomtaka heri afunge ndoa
kuliko kuendelea kuwagonganisha wasanii wa kike.
Kali ya mwaka ni msanii mmoja aliyeshuka kiwango ambaye ni mke wa mtu (tunamsitiri kwa sasa), alipoandika kwamba naye anataka kuonja utamu wa Ray ili ajue kwa nini anagombewa.

No comments:

Post a Comment