Blogger Widgets

November 12, 2013

'Nyawana matashtiti au malkia wa kinyamwezi' Kuzikwa Tabora

Kwa mshtuko na masikitiko makubwa jana nimepokea taarifa ya kifo cha aliyekuwa muimbaji na mtangazaji wa kipindi cha taarab Passion fm Ambaa na mwambao Nyawana Fundikira 'Nyawana matashtiti au malkia wa kinyamwezi'.

Nilimjua Nyawana mara ya kwanza alipokuja Times kwa ajili ya Interview na kutambulisha wimbo wake Niko kamili  kwenye kipindi cha taarab Mitikisiko ya pwani.Alikuwa mchangamfu na mcheshi pia kwa hiyo kifo chake kama binadamu kimenishtua.

Marehemu Nyawana amefariki jana Mwananyamala hospitali alikokuwa kalazwa kwa Ugonjwa wa malaria. Msiba upo nyumbani kwake maeneo ya kwa Bi nyau na taarifa kutoka kwa marafiki zinasema atasafirishwa leo saa 11 jioni kwenda kuzikwa kwao Tabora.