HALI ya mwanamke aliyepigwa risasi na polisi katika Benki ya CRDB
mjini hapa, Violet Lyapa (30) bado ni tete huku taarifa zake zikifanywa kuwa
siri kubwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Selian, Violet bado
amelazwa katika chumba cha
uangalizi maalumu (ICU) huku hali yake
ikibadilikabadilika.
Pamoja na kwamba tukio hilo limechukua siku zaidi ya tano bado hali
ya Violet inafanywa kuwa siri nzito.
Mwanamke huyo amewekewa ulinzi mkali katika wodi aliyolazwa lakini mmoja wa
wauguzi wa hospitali hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini,
amesema hali ya majeruhi huyo imekuwa ikibadilika kiasi cha kulazimika kumpa
uangalizi maalum.
Jeshi la polisi mkoani hapa limekuwa na kigugumizi kutoa taarifa
juu ya tukio hilo na hatua zipi zimechukuliwa juu ya uhalali wa umiliki wa
silaha iliyotumia kuwatishia polisi baada ya kukuta gari lake limetolewa upepo.
Aidha, katika hali inayotia shaka kigogo wa ngazi za juu mkoani
Arusha amekuwa akimjulia hali mara kwa mara majeruhi huyo hasa nyakati za usiku
na taarifa zilizoenea zinasema kigogo huyo ana uhusiano wa karibu na majeruhi
huyo.
Pia, baadhi ya ndugu wa majeruhi wamelalamikia kuzuiwa kumuona ndugu yao na kutakiwa kuonesha vitambulisho.
No comments:
Post a Comment