Blogger Widgets

November 21, 2013

Tazama Pigo walilolipata Kundi la B Heats chini ya Producer Pancho Latino

 Toka wimbo mpya wa Vanessa Mdee ‘Come Over’ utoke wiki iliyopita kumekuwa na fununu kuwa hayuko tena chini ya label iliyokuwa inamsimamia awali (B Hits Music Group), Vanessa aka Vee Money amethibitisha kuondoka katika label hiyo na sasa ana management mpya.
Vanessa-Mdee
Akizungumza katika kipindi cha Showtime New Chapter ya RFA, Vee Money amesema kwa sasa ana management team ya kwake binafsi ambayo ndiyo inafanya maamuzi yote kuhusu muziki wake, kazi ambayo hapo awali ilikuwa ikifanywa na B Hits. Pia amemtaja mtangazaji wa Choice FM, Abby, kuwa ndiye meneja wake kwa sasa.
“Muziki nafanya sasa hivi nafanya independent zaidi niko under management ya kwangu peke yangu….na manager wangu ambaye anaitwa Abby ndio tunafanya all of the decisions kama team.”
Wiki iliyopita Vanessa ametoa single mpya ‘Come Over’ iliyofanywa na producer Nahreel pamoja na Erasto, ikiwa ndio single yake ya pili baada ya Closer.
Hata hivyo mpaka sasa Vanessa hajaweka wazi sababu za kuondoka B Hits, label iliyomtambulisha na single yake ya kwanza ‘Closer’.

KWA UPANDE WA MABESTE
MABESTE KAJITOA KWENYE B’HITZ MUSIC GROUP
Dole singer Mabeste amejiondoa kwenye kundi la B’hitz music group na kusimama kama solo artist. Haijajulikana wazi kwa nini Mabeste amejitenga na kundi hilo la B’hitz.

Katika ukurasa wake wa Facebook Mabeste hajaelezea chanzo cha kwanini hayupo tena katika group hilo la BHITS