Blogger Widgets

February 4, 2014

Check Fumanizi Lililomake HeadLine Baada ya Huyu Mwanamke Kufumaniwa na Mume wa Mtu na Kukutwa kama alivyozaliwa


Sukari hugeuka shubiri pale fumanizi linapochukua nafasi na hiyo ndiyo sababu ya mwanamke anayeitwa Sheila kukiri kwamba mume wa mtu ni sumu kisha kujiapiza kuwa hatarudia tena.

Sheila, alifumwa na mume wa mtu anayeitwa Baba Joyce kwenye nyumba moja ya kulala wageni, iliyopo Manzese, Jumapili (juzi) saa 10 alasiri.


Mapaparazi wetu, walinyetishiwa fumanizi hilo baada ya vurugu kuanza na walipofika eneo la tukio, walimkuta mwenye mume, Mama Joyce anamsulubu Sheila kwa makonde, mateke na vichwa.

Chanzo chetu kilipasha: “Uwazi, nyie si ndiyo mtambo wa kufichua maovu? Njooni huku Manzese kuna fumanizi.”


Baada ya taarifa kufika kwenye dawati, ilichukua dakika 10 kwa mapaparazi wetu kufika eneo la tukio na kuanza kutimiza wajibu wao.

Katika tukio hilo, Mama Joyce alikuwa akimzaba vibao mfululizo Sheila huku akimsindikiza kwa maneno: “Huna haya, unajifanya jirani wakati unamtolea macho mume wangu… ukome kumfuata fuata mume wangu.”


Wakati sekeseke likiendelea, wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni kwa kushirikiana na majirani wachache, walifanikiwa kumtuliza Mama Joyce ambaye baadaye aliondoka na mumewe wakimuacha Sheila analia.

Nusu saa baada ya Baba na Mama Joyce kuondoka, Sheila naye aliaga kwa maelezo kwamba anakwenda kupumzisha akili kwa dada yake anayeishi Mabibo, Dar es Salaam.


SAKATA KAMILI
Habari zinadai kuwa Sheila anaishi jirani na Mama Joyce lakini kwa muda mrefu alikuwa akiwania penzi la Baba Joyce.

“Dunia imegeuka, mwanamke halali anakesha akimuwaza mume wa mtu. Alichokuwa anafikiria ni kumpindua Mama Joyce,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:


“Asubuhi na mapema, Sheila alikuwa wa kwanza kumtumia ujumbe mfupi wa maneno Baba Joyce, akamuuliza ameamkaje na kumtaka awahi kazini. Mume wa mtu unamuuliza hivyo asubuhi asubuhi kweli!”

Inaelezwa kuwa, chanzo cha Mama Joyce kubaini kwamba kuna mchezo mchafu kati ya mume wake na Sheila ni meseji aliyoikuta kwenye simu ya Baba Joyce.

“Baba Joyce alipoamka asubuhi alikwenda kuoga, huku nyuma Sheila alituma meseji inayosema: “Mume wangu mtarajiwa amka uende kazini. Nakupenda sana.”


Madai yanazidi kuwekwa kweupe kwamba Mama Joyce alishikwa na umbeya, hivyo alifungua simu ya mumewe na kusoma ujumbe huo wakati mume wake akiwa bafuni.

“Aliposoma ujumbe huo, ikabidi afungue zaidi na kukuta meseji nyingi za Sheila kwenye simu ya mume wake. Alishangaa sana, kwani walikuwa wanaheshimiana kama majirani,” kilisema chanzo hicho.

Kiliongeza: “Baba Joyce alipotoka kuoga alikutana na maswali kibao, hakuwa na la kujitetea kwani ushahidi kamili Mama Joyce alikuwa nao.

“Baba Joyce alijitetea kuwa hana uhusiano na Sheila isipokuwa mwanamke huyo amekuwa akimtongoza kwa muda mrefu. Mama Joyce hakuridhika, alimwamrisha mume wake amtege Sheila ili amfumanie ndipo atamuamini.

“Alimwambia kama kweli anamtongoza na hamtaki basi amkubali na wakubaliane kukutana gesti ili amfumanie na kumshushia kipigo cha kumkomesha kufuatilia waume za watu.

“Walikubaliana, Baba Joyce alimwita Sheila gesti ili wamalize mambo yao lakini wakiwa wameshavua nguo, Mama Joyce aliingia chumbani na kuanzisha varangati.”


KAULI YA MAMA JOYCE
Alipozungumza na Uwazi baada ya kufuatwa nyumbani kwake, Manzese, Dar alisema: “Shida yangu ilikuwa ni kumtwanga, nimefanikiwa hilo basi. Amemfuatilia mume wangu sana na meseji zake nimeziona kwenye simu. Sitaki zaidi, najua amekoma.”

Baba Joyce hakutaka kuzungumza na gazeti hili kwa madai kwamba yaliyotokea gesti yanamhusu yeye na mke wake.

Kwa upande wa Sheila, hakujibu maswali yote ya waandishi wetu, badala yake alikuwa analia mpaka alipoaga kuwa anakwenda kwa dada yake.
 hii ni kwa mujibu wa global publishers tz