Blogger Widgets

February 13, 2014

Msanii wa Kike wa Bongo Movie Mainda Aja na Mpya Baada ya Kuachwa na Ray


STAA wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kwa sasa hahitaji mchumba wala mpenzi, anahitaji mume wa kumuweka ndani.
 
Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda alisema hata akifuatwa na mtu mwenye fedha nyingi kutaka uhusiano naye, hawezi kumkubalia kwani anachotaka sasa hivi ni ndoa tu.
“Kwa sasa mpenzi wangu ni Yesu na kutokana na yeye mume wangu nimeshamuona kwenye maono…yulee anapiga hodi sura yake,” alisema Mainda.