Blogger Widgets

February 19, 2014

Tazama Picha za Mapigano makali yanayoendelea katika eneo la kwa mzee Juma kata ya Mbezi Juu Dar es salaam

Hili ni kundi la vijana waendesha bodaboda wakienda mtoni kumwokoa mwenzao ambaye wanadai ametekwa na wahuni wanaojificha mtoni na kukaba watu, mpaka sasa boda boda aliyetekwa yupo mwananyamala hospital na mmoja wa vijana wanaoaaminika kwamba ni vibakaba ameshauawa
Kuna mapigano makali eneo la kwa mzee Juma Kata ya Mbezi juu.
Habari zaidi zionasema kwamba Waendesha Bodaboda hao wanaendelea kupambana kwa kutumia silaha za jadi dhidi ya vijana wanaosemekana aidha ni vibaka au wameiba pikipiki ya mwenzao.
Hali ni mbaya majeruhi ni wengi na inasemekana kuna vifo vimetokea.