Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ na mwenyekiti wa Klabu
ya Bongo Movie, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ wameingia kwenye bifu
zito baada ya kutofautiana katika makubaliano ya kikazi.
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni wawili hao waliingia kwenye mabishano wakati Steve Nyerere alipokuwa akiandaa .
filamu yake mpya iitwayo Get Out ambapo alipaswa kumshirikisha Batuli.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alipompigia simu, mwanadada huyo alichomoa baada ya kuona makubaliano ya kifedha hayazungumziwi.
“Batuli alipohoji kuhusu malipo, Steve hakuweka wazi ndipo mambo
yalipoharibika, kikanuka kisha Batuli akamvaa kwa maneno kiongozi huyo
na kudai hana sifa za kuwa kiongozi,” kilisema chanzo chetu.
Ili kujiridhisha na madai hayo, mwanahabari wetu alimwendea hewani
Batuli ambapo alipatikana na kukiri kuwa ametofautiana na Steve chanzo
kikiwa ni filamu hiyo.
“Aliponipigia simu nilimwambia sitaweza kwenda kushuti kwa sababu hakuna
makubaliano yoyote tuliyofanya ikiwemo gharama, usafiri, mavazi na
vinginevyo ndipo akamaindi na kuanza kulaumu na kisha kukata simu,”
alisema Batuli.
Ishu haikuishia hapo, taarifa zinadai kuwa baada ya Steve
kutofurahishwa na majibu ya Batuli, aliendelea kumtumia meseji za
kumlaumu ndipo Batuli alipochachamaa zaidi kwa kujibu mashambulizi.
“Steve anapaswa akasomee utawala na uongozi bora kwani hafai kuwa
kiongozi, hana busara, kwa sababu kabla sijagombana naye nilikuwa
nikisikia maneno na majungu ila baada ya ugomvi wangu na yeye nimegundua
hafai,” alisema Batuli na kuongeza:
“Ananiambia mimi ni msanii mchanga ilihali mimi kwenye kiwanda nipo kwa
miaka kumi na nne na mwaka 2,000 wakati naanza yeye alikuwa anachekesha
watu ili apate kula kwanza nimemdharau kwa sababu amekuwa
akinichonganisha na wasanii wa Bongo Movie eti mimi nimewaambia
wanajiuza.”
Baada ya Batuli kufunguka, gazeti hili lilimgeukia Steve Nyerere na kumsomea madai hayo ambapo alifunguka:
“Sipendwi na watu na sijui nini tatizo, nikiwa kama dairekta nina uwezo
wa kumchagua huyu nifanye naye kazi na huyu kumuacha, yule (Batuli)
kama analeta chuki basi zitakuja hivyo basi ni nyingi tu,’’ alisema
Nyerere na kuongeza:
“Kwa heshima niliyoitengeneza kwa miaka 32 alafu nije nigombane na
mwanamke, kwanza nagombana naye nini? Nashukuru nimepata ushauri,
naendelea na kazi ya kutetea maslahi ya Bongo Muvi kama ni filamu mimi
nilishachezesha msanii mwengine.”
No comments:
Post a Comment