Blogger Widgets

June 5, 2014

Soma Story Ya Msani wa Kike wa Bongo Movie Aliyeamka Asubuhi na Kukuta Kachanjwa Chale Mwili Mzima...Anadai Yalitaka Kumtokea Kama Ya Marehemu Rachel

Mwigizaji mwenye figa ya aina yake Bongo Movie, Tamrina Posh ‘Amanda’. 
MMWIGIZAJI mwenye figa ya aina yake Bongo Movie, Tamrina Posh ‘Amanda’ ameamka na kushtuka akiwa amechanjwa chale na watu wasiojulikana kama alivyowahi kufanyiwa marehemu Recho.
Akizungumzia tukio hilo, Amanda alisema lilitokea siku ambayo dairekta mkongwe nchini George Tyson alipofariki dunia (Mei 30) ambapo hakujua ni nani aliyemfanyia ‘unyambilisi’ huo usiku kwani alishtuka asubuhi na kuona akivuja damu zikiashiria kuchanjwa kwa wembe
Marehemu Recho Haule enzi za uhai wake.
“Nilijikuta nimechanjwa lakini Mungu ni mwema, waliofanya hivyo kama walikuwa na nia mbaya, wameshindwa kwani nilikwenda kuombewa kanisani halitanipata lolote,” alisema Amanda.