Wiki chache baada ya Rapper THE
GAME kutangaza kwamba soon atafunga ndoa na mwanamke aliemzalia
(Tiffney Cambridge), rapper huyo ghafla ametangaza kuahirisha kufunga
hiyo ndoa.
Kupitia page yake ya twitter
yenye zaidi ya watu milioni moja na elfu hamsini, The Game member wa
zamani wa G UNIT ambae alishawahi kuja kupiga show Nairobi Kenya na
kushare stage na Jua Cali, aliandika kwamba harusi imefutwa.
Kasema hiyo imetokana na kosa
alilolifanya yeye na sio huyo mama watoto, ambapo ametoa msisitizo kwa
wanaume wanaopata bahati ya kuwa na wanawake wenye mapenzi ya dhati kama
huyo, wahakikishe hawawaachii.. wawape happy.
Japo hakuna sababu za wazi za
kufutwa kwa harusi hiyo, Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali wa SO SO FRESH ya
CLOUDS FM aliongea kwenye XXL kwamba inaaminika Game kaahirisha harusi
kwa kuogopa kisasi ambacho angeweza kulipizwa na mshkaji ambae wamekua
na beef la muda, mshkaji ambae Game na watu wake 14 walijikusanya na
kwenda kumpiga.
No comments:
Post a Comment