Jean Bedel Bokassa (* 22 Februari 1921 - † 3
Novemba 1996) alikuwa rais na baadaye Kaisari wa Jamhuri ya Afrika ya Kati au baadaye Milki ya Afrika
ya Kati hadi kupinduliwa tar. 21
Septemba 1979.
Bokassa alizaliwa Bobangi
akajiunga na jeshi la kikoloni la Ufaransa. Hadi mwisho wa Vita
Kuu ya Pili ya Dunia alipanda ngazi akafikia
cheo cha afande. Hadi 1961 akawa kepteni. 1964 alitoka katika jeshi
la Ufaransa akaingia katika jeshi la jamhuri changa ya Afrika ya Kati.
Akiwa ndugu wa rais David
Dacko akaendelea kupanda ngazi hadi kuwa mkuu wa
jeshi.
Tar. 1 Januari 1966 Bokassa akampindua rais
Dacko akajitangaza kuwa rais mpya akafuta katiba ya nchi. Bokassa alisaidiwa
mara kadhaa na Ufaransa. Mwaka 1967 aliomba na kupata msaada wa wanajeshi
Wafaransa ili apate kuimarisha utawala wake.
1972 Bokassa akajitangaza
kuwa rais wa maisha. Aliona majaribio mbalimbali ya kumpindua au kumwua
lakini kwa jumla ni wapinzani wake waliopaswa kuaga dunia.
Katikia miaka ya 1970
Bokassa alitafuta usaidizi wa Libya akasilimu baada ya kumtembelea Rais Gadhaffi akajiita Salah Eddine
Ahmed Bokassa.