Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe pointi 42, baada ya kucheza mechi 18, hivyo kujitanua kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi Azam FC kwa pointi sita, ambayo inashika nafasi ya pili kwa pointi zake 36, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wanashika nafasi ya tatu kwa pointi zao 31.
Kagera
inabaki na pointi zake 28 katika nafasi ya tano, baada ya kucheza mechi
19, chini ya Coastal Union ya Tanga inayoshika nafasi ya nne kwa pointi
zake 30.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Simon Mberwa kutoka Pwani,
aliyesaidiwa na Milambo Tshikungu wa Mbeya na Said Tibabimale kutoka
Mwanza, hadi mapumziko, hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la
mwenzake.
Hata
hivyo, mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu
aliikosesha timu yake bao, baada ya kupiga juu ya lango mkwaju wake wa
penalti dakika ya 44.
Refa
Mberwa, alitoa penalti hiyo baada ya Kavumbangu mwenyewe kudakwa miguu
kwenye eneo la hatari na kipa wa Kagera, Mganda Hannington Kalyesebula.
Kipindi
cha pili timu zote zilifanya mabadiliko, Yanga inayofundishwa na
Mholanzi, Ernie Brandts ikiwatoa Kavumbangu na Bahanuzi na kuwaingiza
Jerry Tegete na Mganda Hamisi Kiiza, wakati Kagera inayofundishwa na
mzalendo, Abdallah Kibadeni, iliwatoa Mnigeria Darlington Enyinna na
Julius Mrope na kuwaingiza Paul Ngway na Themi Felix.
Mabadiliko
hayo yaliongeza uhai kwa kila upande na kuongeza kasi na ladha ya
mchezo, lakini bahati hii leo ilikuwa kwa wana Jangwani, kutokana na
kupata bao pekee la ushindi lililofungwa na kiungo wa kimataifa wa
Rwanda, Niyonzima.
Niyonzima
alifunga bao hilo dakika ya 65, baada ya kumhadaa kiungo wa Kagera,
George Kavilla na kufumua shuti kali akiwa umbali wa mita 25,
lililomshinda kipa wa Kagera, Kalyesebula.
Halikuwa
na tofauti sana na bao pekee la ushindi alilofunga kwenye mchezo
uliopita wa timu yake dhidi ya Azam FC, Uwanja huo huo wa Taifa,
Jumamosi iliyopita.
Mshambuliaji
wa zamani wa Simba, Shijja Mkinna alikosa bao la wazi dakika ya 89,
baada ya kupewa pasi nzuri na Paul Ngway, lakini akapiga juu ya lango.
Hiyo
ilikuwa nafasi pekee ya kujutia kwa Kagera ambao leo iliitoa jasho
Yanga. Jerry Tegete naye alikosa bao la wazi dakika ya 87, akishindwa
kuunganisha krosi ya Simon Msuva.
Kwa
ushindi huo, Yanga imelipa kisasi cha kufungwa 1-0 na Kagera katika
mchezo wa kwanza wa ligi hiyo, mwishoni mwa mwaka jana mjini Bukoba.
Katika
mchezo huo, kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu
Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani
Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbangu/Hamisi Kiiza
dk67, Said Bahanuzi/Jerry Tegete dk 67 na Haruna Niyonzima.
Kagera
Sugar; Hannington Kalyesebula, Benjamin Asukile, Martin Muganyizi,
Malegesi Mwangwa, Amandus Nesta, Gaorge Kavilla, Julius Mrope/Paul Ngway
dk 62, Juma Nade, Darlington Enyinna/Themi Felix dk 69, Shijja Mkinna
na Daudi Jumanne.