Blogger Widgets

March 17, 2013

Shilole azungumzia kwa Ndani kwa nini ni "PAKA LA BAA"


MSANII anayefanya muziki wa mduara bongo Shilole huku akiwa anatambulika zaidi kwa jina la ‘Malkia wa mduara’, amesema kuwa safari hii anakuja kivingine kwani anatarajia kuachia mzigo mpya unaokwenda kwa jina la ‘Paka la Baa’, huku akidai kuwa ujumbe unakaopatikana ndani ya kazi hiyo utawagusa zaidi wale wanawake wenye tabia kama za paka anayekulakula ovyo baa.

‘Paka la Baa’ ni yule anayeishi kwa kushida baa na kupenda kula vya bure, huku akiwa hana muelekeo wowote na ndiyo baadhi ya wanawake wa mjini wanavyoishi.


Shilole
alisema kuwa kazi hii imeficha ujumbe mzito unaowagusa baadhi ya wanawake na katika hili anaamini atakayeona ameguswa huyo ndiye atakuwa muhusika wa wimbo huo. .

“Paka la Baa najua tabia zake zinajulikana na kuna baadhi ya wanawake ambao maisha yao ni ya baa na hao ndiyo ninaowagusa hasa, nasema watajuta mwaka huu na wajipange vizuri, najua kuna watu watakuja juu kwani kazi hii itawahusa sana sitaki kuwataja majina lakini wataumia sana,”
alisema Shilole.                              

Shilole kazini



Hata hivyo aliongeza anaamini sasa muziki wake unavuka kimataifa kwani katika show aliyoifanya hivi karibuni Afrika Kusini imekubalika na watanzania wengi walijitokeza kumsapoti kutokana na umahiri wake wa nyimbo za mduara.


Shilole
pia alidai kuwa baadhi ya wasanii wanaotaka kujifananisha naye kwenye upande wa muziki huo, amedai hawana chao kwani yeye ndiye anayejulikana kama Malkia wa mduara bongo kwa mujibu wa mashabiki wake.