Blogger Widgets

December 26, 2012

Breaking News: Padre Ambrose Mkenda apigwa Risasi akiwa maeneo ya Kitomondo Mjini Zanzibar wakati akijiandaa kufunguliwa Geti ili aangie Kwake.

Kwa mujibu wa Breaking News  toka Radio One, Padre anayejulikana kwa jina la Ambrose Mkenda amepigwa Risasi na Watu wasiofahamika kwenye gate la nyumbani kwake wakati akifunguliwa gate aingie nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar, ambako ndiko makazi yake yalipo akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha pekee yake.

Hali yake sio nzuri kwani Risasi aliyopigwa imemdhuru maeneo ya mdomoni.


Waliompiga Risasi Padre huyo inasemekana ni watu waliokuwa kwenye pikipiki, ambao walimvamia akisubilia afunguliwe gate kuingia nyumbani kwake.