Blogger Widgets

May 21, 2013

Check Alichotweet Wayne Rooney Baada ya Mke wake Kujifungua Mtoto wa Kiume

We are family: Wayne and Coleen Rooney, who already have three-year-old Kai, announced the arrival of their second son Klay in the early hours on Tuesday morning
SISI NI FAMILIA: Wayne na Coleen Rooney, tayari wameshatangaza ujio wa kidume chao Klay usiku wa kuamkia leo
Proud father: Rooney revealed the news, with thousands sending their best wishes to the Manchester United striker
HONGERA SANA: Rooney ameandika taarifa hiyo hapo juu katika mtanado wake wa Twita huku maelefu ya watu wakimpongeza na kumtakia kila la heri
Happy days: After going into labour late on Saturday night, Coleen was delighted to announce the arrival of her second son
Over to you David: New United boss Moyes must speak to Rooney about his future after the striker told retiring manager Sir Alex Ferguson that he wanted to leave Old Trafford
JUU YAKO DAVID:  Kocha mpya wa United Moyes lazima azungumze na mshambuliaji huyo baada ya kumueleza bosi wake Sir Ferguson kuwa anaomba kuihama United.

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mshambuliaji nyota wa klabu ya Manchester United, “Mashetani wekundu” na mabingwa wa ligi kuu soka England, Wayne Rooney amepata mtoto wa pili usiku wa kuamkia leo.
Mke wake mpendawa Coleen  amejifungua mtoto wa kiume na wamempatia  jina la Klay.
Coleen alipatwa na uchungu jumamosi usiku  wiki iliyopita na kumsababisha Rooney ashindwe kusafiri na timu yake kuifuata West Bromwich katika kipute cha kufunga pazia la ligi kuu England ambapo mechi hiyo ilimazika kwa sare ya kufungana mabao 5-5 na kumuaga rasmi kocha wa klabu hiyo Kibabu Sir Alex Ferguson.
Rooney alitangaza taarifa hiyo katika mtandao wake wa Twita akiwaambia wafuasi wake zaidi ya milioni 6 kuwa  amefurahi kupata mtoto mzuri wa kiume Klay Anthony Rooney, huku mama yake na mtoto Klay wakiwa wazima.
Mtoto wa kwanza wa Rooney ana miaka mitatu mpaka sasa na anaitwa Kai, hivyo sasa amekuwa baba wa watoto wawili. Hongera sana Rooney.
Wakati huo kuna taarifa kuwa kocha mpya wa United, David Moyes anatarajia kukutana muda wowote na Rooney ili kuzungumzia hatima yake klabuni hapo msimu ujao.
Hivi karibuni Rooney na Ferguson hawakuwa katika maelewano mazuri mpaka nyota huyo aliomba kuihama klabu yake hiyo ambayo imempa jina kubwa zaidi duniani.

No comments:

Post a Comment