Blogger Widgets

May 23, 2013

Jini Kabula Apasua Jipu Kuhusu "Jack wa Chuz" Kwa Tabia Yake ya Kuiba Waume za Watu

 
 Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’.
 MASTAA wanaunda Kundi la Scorpion Girls, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na Isabella Mpanda ‘wamemtapika’ mwenzao, Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’ katika kundi lao.
mujibu wa chanzo makini, mastaa hao wameamua kumuengua Jack Chuz kutokana na tabia zake ikiwemo ya kubadilisha mabwana na kuiba waume za watu.
Alipoulizwa Jini Kabula juu ya taarifa hizo, alitiririka:

 
Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
“Tumemtema Jack Chuz kutokana na tabia yake ya kupora waume za watu, hata miye alishawahi kuniibia Chuz (Tuesday Kihangala) tena nikiwa na kichanga, nasema kutoka moyoni simpendi Jack.”
Akijibu sakata  hilo, Jack wa Chuz alisema:
“Jini Kabula na Isabella hawana uwezo wa kuniondoa kundini kwa sababu hawana mamlaka, ninachokijua mimi bado niko kwenye kundi hilo.”