Blogger Widgets

May 4, 2013

Soma Interview aliyoifanya Penny wa Diamond Huku akipaniki na Kusema Hana na Haijui Hiyo Mimba ya Diamond wanayoizungumzia


Mwanamziki anayefanya vizuri kwenye gemu ya Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ siku za nyuma alitoa kauli ya kuwa mchumba wake ambaye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ ana ujauzito wake na kwamba amemnunulia ‘mkoko’ (gari) la mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kwenda nalo kliniki kama utakuwa mfutaliaji mzuri wa story zetu basi utakuwa umeshaisoma hii sasa Penny ameifungukia kauli hiy
Baada ya penny kulizwa juu ya ujazito wa Mwanamziki Diamond alioneka kushangzwa sana na kauli hiyo na kupaniki ghafla
Alisema amekuwa akisoma habari za ‘mimba’ yake kupitia magazeti lakini hajawah kuulizwa na mwandishi yeyote, jambo linalomshangaza sana.
Na hivi ndivyo ilivyo kuwa katika maongezi na mwandish kutoka GPL
Penny alisema: Namshangaa! Ni mimba ipi kwanza?uhusiano wangu na Diamond unaninyima raha kutokana na maneno ya watu.
Penny: Mh! Yaani sijui hata niseme nini, nashangazwa sana na hizi habari, nazisikia tu halafu mimi mwenyewe mhusika sijapewa nafasi ya kuzungumza.
Unajua sijazoea maisha haya ya kila wakati kuzungumza na waandishi. Naomba mniache, nani aliwaambia kuwa mimi nina mimba?
Funguka: Diamond.
Penny: Kama ni Diamond muulizeni yeye mwenyewe! Mbona nakosa raha jamani?
Funguka: Vipi mna mpango wa kuoana na Diamond?
Penny: (kwa hasira) Hizo ni ishu zangu binafsi, kama tutaoana au hatuoani ni mipango yetu, sioni sababu ya kutangaza kwenye media.
Funguka: Unaichukuliaje kauli ya mama mkwe wako, yaani mama Diamond? Inadaiwa alisema hatambui uhusiano wowote wa mtoto wake na mwanamke mwingine hadi atakapofunga ndoa.
Penny: Tafadhali sana, sitaki kuzungumzia habari kuhusu mama Diamond. Kwa hilo ‘no comment.’
Funguka: Vipi lakini, unainjoi kuwa na uhusiano na Diamond?
Penny: (Akakata simu).
Funguka: Haloo… haloo!
Hata hivyo mapaparazi wetu walipojaribu kumpigia simu tena hakupokea licha ya kuita kwa muda mrefu mpaka kukatika yenyewe
From:GPL