Blogger Widgets

May 17, 2013

Tamko la Ney wa Mitego Baada ya Nick Mbishi Kuandika Wimbo Unaoitwa "NEY WA MITEGO" Mtoto Mzuri

Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya Ney Wamitego amesema Nikki Mbishi na wasanii wengi wachanga huwa wanajaribu kuwa-diss wasanii wakubwa kwa lengo la kupata jina.
Ney alizungumza hayo pale nilipotaka kujua kutoka kwake juu ya kitendo cha msanii Nikki Mbishi kutengeneza wimbo unaoitwa Ney Wamitego, wimbo ambao unaonekana moja kwa moja unamzungumzia Ney Wamitego kama mwanamke au mwanaume siyo.
Mwanzoni mwa mazungumzo yangu nilitaka kujua kutoka kwa Ney, anachukuliaje kitendo cha msanii huyo kuandika wimbo unaomzungumzia yeye, Ney alikataa kuzugumza hilo huku akisema "Yaani kaka mimi nikiongea kitu tu mimi nampa kick ile anayotaka yule dogo, mi sitakiwi kuongea kitu, yaani hiki ndio kitu ambacho watu wa karibu wamekuja wameniambia this time huyu amefanya hiki kwa sababu ya hiki, so dont talk anything"
From: fununuhabarii

No comments:

Post a Comment