Blogger Widgets

July 15, 2013

Hapa Ndipo walipofikishana Diamond Platnum na Irine Uwoya Mpaka Kusababisha Irine Uwoya Kumwaga Chozi

SAKATA LA DIAMOND NA UWOYA ,UWOYA AMWAGA CHOZI

Irene Uwoya.

KUFUATIA habari iliyoripotiwa na gazeti tumbo moja na hili, Amani wiki iliyopita, ikiwa na kichwa cha ‘DIAMOND AFICHUA KISA CHA KULALA NA UWOYA!’, mwigizaji Irene Uwoya amemfungukia mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa kitendo chake cha kuanika uhusiano wao.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Uwoya, baada ya habari hiyo kuingia mtaani na kuzua gumzo kubwa, mwanadada huyo alishindwa kupiga misele mjini na kujikuta akiwaza hadi akamwaga chozi akijuta kuwa karibu na Diamond.
Baadaye Uwoya aliamua kuzama kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuandika:NA GPL

“Kuna saa najiuliza kwa nini ukimwamini mtu ndiyo anakugeuka...kwa nini ukiwa muwazi watu wanakuchukulia vibaya?
“Leo nimeumia sana kuliko siku zote...sijaamini mtu niliyemwamini kumuona kama rafiki yangu anaweza kuongea sh*t kuhusu mimi...au najiuliza siruhusiwi kuwa na rafiki wa kiume?
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
“Lakini saa nyingine nakaa chini nasema God ...u know me better.”
Uwoya alipoandika maneno hayo ikawa kama amechochea kuni kwenye moto ambapo mashabiki wake walimshambulia kwa maneno makali kuwa aliporipotiwa mara ya kwanza na gazeti hili alikanusha sasa mbona mwenzake kaanika ukweli?
Uwoya na Diamond walidaiwa kuwa ‘wanatoka’ kwa muda mrefu na walifanya jitihada za hali ya juu kuuficha ukweli kuhusu uhusiano wao lakini ilipofika Machi 25, mwaka huu, gazeti hili liliwanasa chumbani katika hoteli moja iliyopo Mbezi Beach ufukweni mwa Bahari ya Hindi, Dar.