Blogger Widgets

July 17, 2013

Hii Ndio Bahati aliyoipata Izzo Bizness Mpaka Kumshuru Jokate Kidoti


  Siku chache tuu zimepita tangu video ya Love Me ya Izzo Bizness ambayo amemshirikisha Barnabas na Shaa kuachiwa kwenye vituo mbalimbali vya TV hapa Bongo. Video hiyo imepokelewa vizuri na waTZ wengi.
Sasa Rapper huyo amemshukuru Mungu kwani Video yake hiyo imepitishwa kwenye kituo kikubwa cha TV Africa, Channel O. Kupitia kwenye mtandao wa Twitter, Izzo aliandika:


Hata hivyo Izzo Bizness amesema, ngoma hiyo haijaanza kupigwa. Pia amekiri kwamba video zake nyingi alizipeleka kwenye Channel O lakini hazikupitishwa kutokana na kutofikia kiwango kinachohitajika, hivyo kupitishwa kwa Love Me kumempa furaha.

Love Me imefanywa na E-Media chini ya Director Nick Dizzo. Unaweza ukaitazama video hiyo kali hapa.