Blogger Widgets

July 19, 2013

Picha Mbalimbali za Msanii Wastara Akionekana Location Kutoa Movie Yake Baada ya Kupata Matatizo Mbalimbali Ikiwemo Kufiwa na Mume Wake Sajuki


  
Hatimaye mwadadada Wastara Sajuki amerejea tena kwenye ulimwengu wa filamu baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye tasnia hii kutokana na matatizo aliyoyapata ya kuondokewa na mumewe Juma Kilowoko (Sajuki) mnamo mwezi wa January mwaka huu.
Akizungumza katika utengenezaji wa Filamu yake mpya ya kwanza atakayoiachia wastara amesema Filamu hii mpya wastara amesema kuwa itahusu maisha ya kawaida ya mwanadamu na jinsi ambavyo matatizo yanayomkabili binadamu yanavyoweza na kumuathiri kisaikolojia na kumpelekea kufanya mambo ambayo hakuwai kuyafikiria.


Wastara amesema kisa kikuu kwenye filamu hii yake mpya ni jinsi familia moja iliyokuwa na maisha mazuri na baadaye mama wa familia kupata kansa ya kizazi na kupelekea kuondelewa kizazi chake kabla ya kufiwa na mtoto wake pekee aliyekuwa naye na namna ambayo mumewe anavyojaribu kumliwaza mkewe kwa matatizo hayo yanayotokea.
Wastara amesema kuwa kwenye Filamu hii ameshirikia na waigizaji Yusuph Mlela na Nisha pamoja na mwigizaji mweingine aliyemtaja kwa jina la Hamida na amewataka wapenzi wake wote wakae mkao wa kula kwa ajili ya Filamu hii inayotarajiwa kutoka mwezi wa tisa.CHANZO BONGO MOVIE