Blogger Widgets

July 12, 2013

Picha Mbalimbali Za Video Iliyomuonesha Wema Sepetu akiwa anapigwa Denda Live na Jamaa aliyekuwa Nae Huku akiwa anavuta Sigara

 
Video inayomuonesha staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akidendeka na mwanaume imevuja mtandaoni...

Haikuweza kufahamika mara moja lengo la Wema na mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Aidany ‘kujishoot’ wakifanya vitendo hivyo ila wanaonekana wakiwa katika mazingira ya ki-Mr & Mrs.Aidha, katika video hiyo, Wema anaonekana kutumia nguvu kubwa kumshawishi Aidany amsogezee mdomo lakini mwanaume huyo anasita na hata alipokubali kudendeka hakutoa ushirikiano wa asilimia 100.


Mwanaume fegi mkononi
Katika video hiyo, mwanaume huyo anaonekana kutumia muda mwingi kuvuta sigara yake huku Wema akiwa bize kumpapasa kimahaba.


Ni filamu?
Baada ya video hiyo kunaswa swali lililokuja ni je, ni sehemu ya filamu za mwanadada huyo anayemiliki Kampuni ya Endless Fame au ni uhalisi wa mambo!

 Katika kujua ukweli, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Wema kupitia simu yake ya mkononi lakini mara nyingi imekuwa ikiita bila kupokelewa.

Aidha, mwandishi alichukua hatua ya kwenda nyumbani kwake maeneo ya Kijitonyama jijini Dar lakini alimkosa na hata alipokwenda ofisini kwake hakuweza kumpata.