Blogger Widgets

August 11, 2013

CHECK PICHA:Maiti Yakurupuka kutoka Katika Jeneza na Kumpora Muombolezaji Chupa ya Maji, Kiu "Chamfufua"


Wapita Njia walipata hali ya  kutishwa wakati mtu huyo, ambaye alisemekana kuwa maiti, ghafla aliamka na kumpora mmoja wa waombolezaji chupa ya maji na kuanza kunywa.


Raia huyo wa China alidanganya kifo chake mwenyewe ili kuishitaki serikali baada ya mabishano na wafanyakazi wa serikali ambao inasemekana walimpiga, basi akafanya uongo huo ili apate fidia ya Kifo hicho.

Lakini mpango wake uliingia dosari kutokana na Hali ya Joto Kali katika Mkoa wa Hubei, Huko China ya kati. 


Tukio hilo lilitokea majira ya saa Kumi Alasiri wakati zaidi ya watu 10 wakiwa wamembeba maiti huyo huku akiwa kufunikwa na karatasi nyeupe karibu na kituo cha Jianghan Road Subway katika mji mkuu wa mkoa wa Wuhan. 


Zaidi ya watu 300 waliokusanyika katika eneo la tukio, na maafisa wa polisi 80 walipelekwa eneo la tukio ili kudumisha amani. 


Baada ya masaa mawili ya maandamano, "Maiti" Mtu huyo ghafla alisimama, akaipora chupa ya maji ya kunywa na  kusema: "Ni Joto sana, siwezi kuvumilia ". 


Maiti huyo aitwaye Han, pamoja na wenzake wawili wengine, wamekamatwa kwa kitendo chao hicho.