Blogger Widgets

October 29, 2013

Mtazame Sasa Msanii wa Bongo Movie "CHOPA" Akiwa Kwenye Mavazi ya CCM na Kutangaza Nia ya Kugombea Ubunge

Yule msanii wa vichekesho nchini alialeta msemo wa alimashauri ya kichwa bwana juma chikoka alimaarufu kwa jina la chopa mzee wa halimashauri ya kichwa bado ameonyesha kutokukata tamaa katika harakati zake za kuelekea mjengoni mara atakapotwaa kiti cha ubunge.

Chopa ambaye mwaka 2010 aligombea kiti hicho kwa tiketi ya ccm wilaya ya ilala lakini kura hazi kutosha hivyo akawa kashindwa kuendeleza harakati zake za kuingia mjengoni hivyo kwa sasa chopa ameibuka tena na kusema kuwa bado nia nguvu na hari ya kugombea ubunge anavyo na ana uhakika safari hii ni ushindi wa kishindo.

                           
Ujumbe waa chopa katika instagram unasomeka hi ......2010 nligombea ubunge lakin kura hazikutosha,sijakata tamaa na sitakata tamaa ktk mbio za kufikia ndoto zangu, japo kuna watu wazito wameanza mbinu chafu dhidi yangu,wakiendelea ntawataja hadharani..MUNGU nijaalie afya,uwezo, na ujasiri na nguvu koz naamin akuna kinachoshindika kikubwa ni uzalendo,uwezo,mipango na mbinu..aliandika chopa kupitia mtandao wa instagram
Baada ya kuona ujumbe huo thesuperstarstz ilimuendea hewan bwana chopa kutaka kujua ukweli wa jambo hili ambapo chopa alisisitiza kuwa bado ana dhamira ya kweli na atahakikisha anachugua kiti cha ubunge muda ukifika,pia chopa amekiri kufanyiwa hujuma kali ili asishinde na kusema kwasasa hatawavumilia tena kama kipindi kile kwahiyo waache mara moja kumuhujumu la sivyo ataweka majina yao hadharani kwakuwa ushahid anao tena wa kutosha.Mimi bado nina dhamira ya kweli na nina uhakika nitachukua safari hii japo kuna watu wanatengeneza zengwe juu yangu  lakini nawaambia hawataweza walifanikiwa kipindi kile na mm kwakuwa ni mzalendo nilikaa kimya ila kwa sasa nawaonya wasiendelee na harakati hizo maana muda si mrefu kama wataendelea basi nitayaanika majina yao na hatua kali za kisheria zitafuata kwani ushahidi ninao ila nataka tuwe ndugu wa kweli kwanza alisema bwana chopa.