Blogger Widgets

October 9, 2013

Soma Ukweli wa Mrisho Ngasa Kuoa Mke wa Tano.Ni Aliyekuwa Mwanafunzi wa CBE


 Mchezaji nyota aliyekuwa kwenye kifungo cha kutocheza mechi sita kisha kulipa faini ya shilingi milioni 45 kwa timu aliyokuwa anaichezea awali ya simba siku za hivi karibuni alitangaza kuwa mshabiki wake na wadau wamchangie pesa kwa ajili ya kufidia pesa aliyolipishwa na club ya simba ambayo kwa mujibu wa ngasa kuwa pesa hiyo ilitoka mfukoni mwake lakini kumbe wiki ijayo anaoa mke mwingine na kufuatiwa na bonge la sherehe.

Habari za uhakika zilizofika mezani kwa Xdeejayz na kufanyiwa upepelezi wa hali ya juu zilisema kuwa mchezaji huyo sasa hivi yuko kwenye vikao cha siri kwa ajili yaa maandalizi ya kuoa msichana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la  Rebeka ambae alikuwa chuo cha CBE Mwanza.Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa msichana huyo ameachishwa chuo na Ngasa na sasa hivi anaishi hapa mjini Dar na huenda wiki hii au ijayo wakafunga ndo” Habari ndo hiyo Ngasa anaoa lakini tukio hili analifanywa kwa siri kubwa sana hataki mtu yeyote ajue hata timu yake hapendi wafahamnu na ndio maana anafanya kwa siri kubwa” Alisema dada huyo
Ngasa ambae inadaiwa sasa hivi amekuwa akishikiria rekodi ya kufungua ndoa nyingi kuliko mchezaji yeyote na huyu mke wake huenda akawa wa wanne na hao ni wale wanaotambuana lakini inadaiwa bado kuna wengine pembeni ambao mchezaji huyo amewaongezea idadi.


Hata hivyo papalazi wa Xdeejayz alifanya juhudi za kumtafuta Ngasa kupitia simu yakeya kiganjani lakini kwa bahati mbaya lakini hata hivyo blog hii inawaahidi wasomaji wetu kuwa tutahakikisha tunazama kwenye sherehe hiyo hata kama ikifanywa kwa siri na tutaweletea picha za tukio zima zenye ushahidi wote.

source:
Xdeejayz