Blogger Widgets

November 12, 2013

PICHA MBALIMBALI:Mzee wa miaka 103 afunga ndoa na bibi wa miaka 99!

Sikiliza story hii inayowahusu wapendanao wenye asili ya Paraguay waliokutana na kupendana mwaka 1933, miaka sita baada ya vita ya pili ya dunia.Miaka 8 baadaye waliamua kuishi pamoja kama mke na mume.

Jose Manuel Riella 103 na Martina Lopez mwenye miaka 99 wamefunga ndoa na kuungana pamoja katika sherehe iliyohudhuriwa na wanafamilia yaani watoto wao 8,wajukuu 50,vitukuu 35 na watoto wa vitukuu (sijui wanaitwaje lol) 20!
Wageni walitokwa na machozi ya furaha waliposhuhudia vikongwe hao huku Mr. Riella akiwa kwenye wheel chair ametinga suti nyeusi na shati la dark blue alikuwa akitabasamu kila akimtupia jicho mkewe aliyetinga gauni refu jeupe la harusi

Baada ya hapo ikadondoshwa party na kiongozi wa dhehebu la katoliki aliyesimamia shughuli alisema ni wanaharusi wapya wakongwe sana ambao hakuwahi kuozesha kabla.