Blogger Widgets

November 2, 2013

Picha:Lulu atoa msaada wa pesa kwa wagonjwa wa Saratani katika hospitali ya Ocean Road

 75a4dc9a42c411e3b01422000aaa05b1_8

 Muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu amewatembelea wagonjwa wa saratani waliolazwa kwenye hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam leo na kuwapa msaada wa pesa ili ziwasaide kwa matibabu na mahitaji mengine.


Kupitia Instagram, Lulu aliwataka Watanzania wawe na utaratibu wa kuwasaidia wagonjwa wa aina hiyo kwa chochote walichonacho.

“Naamini mimi sio mwema sana mpaka Mungu akaniwezesha kuona mwezi huu nikiwa mzima na mwenye afya. kwa kutambua hilo nimeanza mwezi huu kwa kupita katika hospitali ya Ocean Road na kutoa mchango ili kuwasaidia wagonjwa wa CANCER na tuwe na utaratibu wa kuwakumbuka wahitaji kwa chochote tulichonacho,” aliandika.