Blogger Widgets

November 8, 2013

Tazama Picha Mbalimbali Zikonesha Movie Kali Inayokuja Ikiwa Joketi Kidoti Ndio mhusika mkuu kwenye filamu ya JB ‘Mikono Salama’, wapo pia Irene Uwoya na Richie

Baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuigiza filamu, mrembo na mtangazaji, Jokate Mwegelo ameigiza kwenye filamu iitwayo ‘Mikono Salama’ akiwa pamoja na Irene Uwoya na Single Mtambalike maarufu kama Richie.
IMG_6269 (600x400)
John Kalaghe, Irene Uwoya, Richie na Jokate wakiwa location

Kwenye filamu hiyo ya kampuni ya JB, Jerusalem Film Company na iliyoongozwa na Adam Kwambiana na John Kalaghe, Jokate ameigiza kwa jina la Ndekwa.
IMG_6240 (600x400)
Jokate na Richie

“Richie ameigiza kama rafiki yake na kaka yangu ambaye anatoka vilevile na wifi yangu na baadaye ananitaka mimi na tunaishi pamoja lakini vitu haviendi sawa,” Jokate ameiambia Bongo5.
“Wifi yangu atakuja na atakuwa anamtishia maisha sababu yuko na mimi. So kidogo yupo kama half my boyfriend, half my protector but sio mtu ninayempenda.”
IMG_6259 (600x400)
Irene Uwoya ndiye aliyeigiza kama wifi yake na Jokate kwenye filamu hiyo

Jokate amesema wakati wa kushoot filamu hiyo alikuwa akijikuta akichoka mno kwakuwa hajaagiza kwa kipindi kirefu na shughuli ilikuwa ikichukua siku nzima na nusu.
IMG_6265 (600x400)


Irene, Kalaghe na Jokate ama Ndekwa

“Naweza nikaondoka home saa moja, narudi saa 10 usiku kwahiyo nilikuwa nachoka sana. Nilikuwa nafanya kazi sana, kwangu mimi kidogo ilikuwa inanisumbua. Lakini watu katika kampuni ya JB walikuwa wakiniattend vizuri, nikichoka wanasikiliza, nakula nini, maji whatever kwahiyo at least walinipa wepesi katika kucheza character yangu.”
IMG_6343 (600x400)
Adam K, Jokate na Kalaghe

IMG_6338 (600x400)
IMG_6340 (600x400)