Blogger Widgets

December 31, 2012

Hii Ndio Funga Mwaka Hamna Nyingine:Haya Ndio Majimama Mwili yaliyokutwa na Camera za GPL yakifanya mashindano ya nani mwenye Makalio makubwa

Mijimama miwili, Mwajuma Thabit ‘Rose Jimama’ (kushoto) na Fransisca Mbena ‘Chuma’ hivi karibuni ilinaswa na paparazi wetu ikishindana kuwa nani ana makalio makubwa kuliko mwenzake bila kujali watu waliokuwa wakiwakodolea macho.

Mijimama hiyo ilikutwa na paparazi wetu ikifanya kufuru hiyo Jumapili ya Agosti 21, mwaka huu nje ya nyumba moja iliyopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam.
 
Baadhi ya wapita njia walipowaona wanawake hao ambao ni wake za watu, wengine walifurahia huku baadhi wakionesha sura za kushangaa na kuhoji, kulikoni watu wazima kama hao kufanya vitendo vya ovyo?

Kufuatia tukio hilo, mpigapicha wetu alizungumza na mmoja wao ambaye alisema walikuwa kwenye maandalizi ya shindano la Mwanamke Nyonga linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam siku ya Iddi Pili.

Jimama hilo lilisema wameanza mazoezi mapema baada ya kusikia kuwa, katika mpambano huo kutakuwa na mijimama mingine iliyokubuhu kwenye masuala ya unyago, hususan mambo ya nyonga.

“Tumeamua kufanya mazoezi mapema kwa kuwa tumesikia wenzetu tunaokwenda kushindana nao ni mijimama ya nguvu na mambo yao si mchezo,” alisema Mwajuma.