Blogger Widgets

December 13, 2013

Muoneakano Mzima wa Kina Mama Waliojotokeza Kumsaidia Mwanamke Mwenzao Aliyejifugulia Barabarani Baada ya Kukamatwa na Uchungu Njiani

Akina mama waliomsaidia mama Eric kujifungua wakiwa na mtoto aliyezaliwa.
MWANAMKE anayefahamika kwa jina la mama Eric, hivi karibuni muda wa saa 11jioni alijikuta akijifungua mtoto wa kiume Barabara ya Posta jijini hapa kufuatia kushikwa na uchungu ghafla.

Akiwa katika hali ya kuhangaika kusukuma mtoto, mwanamke huyo aliishiwa nguvu huku tayari kichwa cha mtoto kikiwa kimetokeza nje, ndipo mama mmoja aliyekuwa akisafiri akajitokeza kumsaidia kumzalisha.

“Nilimwona akihangaika kusukuma mtoto, lakini akaishiwa nguvu. Nilimwonea huruma nikatua begi na mkoba, nikamshika mikono akaja mama mwingine tukasaidiana kumzalisha,” alisema mama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Euphrazia John, mkazi wa Bariadi, Simiyu.
Euphrazia alisaidiana na akina mama wengine, Juliana Wambura na mke wa diwani wa zamani wa Kata ya Nyamagana, Mama Mkiwa.

Mama Eric akiwa kwenye gari kuelekea nyumbani