Blogger Widgets

December 24, 2013

Picha: Diamond aionesha kwa mara ya kwanza video ya ‘Number One-Remix’ akiwa na Davido Msani wa Nigeria kwa watoto waishio kwenye mazingira magumu

dp-1dp-1 
Mashabiki wengi wa Diamond Platnumz wanaisubiri kwa hamu kuiona Video ya ‘Number One-Remix’ iliyompeleka nchini Nigeria mwezi uliopita, lakini mwimbaji huyo aliyetambulisha style yake ya ngololo ameamua kutoa heshima kwa watoto waishio kwenye mazingira magumu kuwa wa kwanza kuitazama video hiyo.
dp-1
Wiki iliyopita Naseeb Abdul alitembelea watoto waishio kwenye mazingira magumu hapa Dar es salaam, na mbali na misaada aliyoitoa aliweza pia kuwaonesha video hiyo iliyoongozwa na director mkubwa wa Nigeria na Afrika kwa ujumla Clarence Peters.
dp-2
Platnumz ameshare picha hizo akiwa na watoto hao katika blog yake This Is Diamond na kuandika
“Kama nilivyotangulia kusema awali kuwa,hawa watoto ndiyo mashabiki wetu wakubwa,na mara
nyingi hawapati fursa ya kuhudhuria maonyesho yetu ama kukutana na sisi..hivyo kutokana na kuwa awali,video ya number 1 version ya kwanza niliizndua kwa baadhi ya watu special pekee..awamu hii,video ya number one remix niliyoifanya na Davido wa Nigeria..nimeamua kuionyesha kwa mara ya kwanza kwa watoto waishio katika mazingira magumu..usisahau pia kuwa tarehe 25 mwezi huu.mchana .pale Leaders club nitakuwa na tamasha special kwa ajili ya watoto ambao wengi hawapati fursa ya kuona maonyesho yetu..na siku hiyo hiyo usiku tutakuwa Mwanza..get ready …”

dp-4
dp-5