Blogger Widgets

January 9, 2014

Maneno Ya Joyce Kilia Kuhusu Shutuma Ya Zitto Kabwe na Mtazamo wake Juu ya Chuki ya Mh Mbowe

NGUVU YA ZITTO IMEMUINGIA HADI MKE WA JUNIO KILEO,KILEO NI YULE AMBAE ALILALAMIKIWA NA KUSHITAKIWA NA ZITTO KUWA ALIWEKA KWENYE MTANDAO WAKE HABARI ZA KUWA ZITTO KAONGWA NA CCM

MKE WA KILEO BI JOYCE KIRIA AAMUA KUANIKA UKWELI HADHARANI

Dada Joyce Kiria ambaye ni mwendesha kipindi cha Wanawake Live CHA EATV
Haya ndiyo maoni yake katika mjadala mmojawapo katika wall ya Albert Msando. Mjadala upo chini ya Kitila na Mwigamba wavuliwa uongozi.
"Kama CDM mmeamua kuchonga barabara, msiwaache wanaokwenda kinyume na Miiko na Maadili ya Uongozi. Mh Mbowe kazaa nje ya Ndoa! Mh Mukya kazaa na Mume wa mtu. HAO NI VIONGOZI WA AINA GANI??

Na Viongozi wengine wenye tabia za namna hiyo hawafai hata kuwa wajume wa nyumba 10...


CDM Mkiishia kwa ZZK mtakuwa Mmebagua sana. Na mtakuwa mmewaonea sana kina ZZK na his Team. Mtazamo tu


Yangu Macho...


Uaminifu ndo Msingi wa mambo yote! Ukishindwa kuwa mwaminifu kwenye familia yako, Ndoa yako, nyumbani kwako, hakuna mahali pengine utaweza kuwa Mwaminifu.


Hayo ya Ufisadi yanaanza na Mtu binafsi, Familia, ( Mke) na mwisho ndo Jamii...


Umeshindwa kuongoza Familia yako, ivi kweli Taifa ndo Utaliweza??


CDM msipokubali chujio liwapitie wote, mkabakia kuangalia tabaka na vidagaa mtachelewa sana kufika....


Mtazamo wangu na Msimamo wangu ndo huo...


Uchaguzi ujao ni heri kuchagua Mtu siyo chama! kama mambo hayatabadilika...


Note: Jazba inatoa watu povu kweli..mie huwa sijali


Hiyo inaitwa Vunja Ukimya, Elimika,


Uaminifu wa Kiongozi yeyote na dhamira yake ya kubeba Dhamana ya Matumaini ya Wananchi Ni Lazima Ianzie nyumbani kwake.


Kama Kiongozi ameshindwa kutunza Uaminifu kwa Mke wake, (familia moja) atawezaje kwa jamii (familia lukuki) kama Kiongozi ameiumiza familia yake ya watu wachache, atashindwa vipi kuwaumiza watanzania wengi asiowajua....


Unapomuumiza Mke wako aliyekuzalia Watoto, kwa kutoka nje ya Ndoa, tena Ukazaa huko!! wewe huna tofauti na Mafisadi wengine...


Hufai Kuwa Kiongozi hata wa Nyumba 10....


Huo ndo msimamo wangu mimi Joyce Kiria..... Tokeni povu lakini hamnisumbui ng'o... Ukweli daima nitasema ili niepuke Unafiki na Uzandiki niwe Huru...."