Blogger Widgets

April 22, 2014

Picha Jinsi Kamanda Alivyofumwa na Mke wa Mtu Gest Tabata akiwa na Radio Call Yake


KAMANDA wa kampuni moja ya ulinzi ya jijini Dar es Salaam (jina tunalo), Japhet Misana ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha mafunzo cha kampuni hiyo, Alhamisi iliyopita wakati Wakristo wakiwa kwenye hekaheka za Sikukuu ya  Pasaka, alinaswa gesti akiwa na askari wake ambaye ni mke wa mtu.
 
Kamanda akiwa katika hali ya sintofahamu baada ya kunaswa akiwa na askari wake ambaye ni mke wa mtu.
Kamanda huyo na askari wake (jina tunalo) walijichimbia kwenye gesti hiyo iliyopo Tabata Matumbi, Dar kwenye chumba namba 6.
 
Kamanda wa kampuni ya ulinzi, Japhet Misana akivaa baada ya kunaswa akiwa na mke wa mtu.
Ilidaiwa na chanzo chetu kuwa, kamanda huyo alianza kutokwa na ‘mate’ ya matamanio kwa askari wake huyo tangu alipofika kwenye kampuni hiyo kuomba kazi.
 
Akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, askari huyo alipewa kazi kwa sharti la kutoa ‘burudani’ kwa kamanda huyo lakini baada ya kufanikiwa kupata ajira alianza kumpiga danadana mkubwa wake huyo kuhusu suala la ‘majamboz’ kama walivyokubaliana.
 
“Wakati danadana zikiendelea wapambe walimng’ata sikio mwenye mali kwa kumwambia kwamba asiwe ‘babu jinga’ kwani mali zake zinakaribia kuliwa na wapenda vinono,” kilisema chanzo.
Taarifa hizo, kwa mujibu wa chanzo, zilimshtua sana mwanaume huyo ambaye alianza kumwekea mtego mkewe pamoja na bosi wake kwa kumkabidhi kazi hiyo mdogo wake kuwa ‘shushu’.
Siku ya Alhamisi Kuu ambayo kimvua kilisumbua karibu jijini zima la Dar sanjari na kibaridi, shushu huyo alimsikia shemeji yake akizungumza kwenye simu na mtu mmoja aliyehisiwa kuwa ndiye kamanda wakiahidia kukutana kwenye gesti hiyo.
Shushushu huyo haraka alipiga simu kwenye chumba cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) na kuwaeleza mchezo mzima.Baada ya kupata taarifa hizo bila kuzubaa, makamanda wa OFM walitumia dakika zisizozidi 10 kutoka makao makuu ya ofisi zao zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar na kuwasili eneo la tukio.
OFM na shushu huyo waliwaona wawili hao wakiongozana na kupiga kona kadhaa kisha wakaingia kwenye gesti hiyo na kujichimbia kwenye chumba namba sita.Wawili hao wakiwa chumbani makachero wa OFM waliwasiliana na askari Polisi wa Kituo cha Tabata ambao nao waliwasili bila kuchelewa.
Walipofika waliingia ndani ya gesti hiyo na kumtaka mhudumu, walijitambulisha na kumweleza kilichowaleta pale ambapo mfanyakazi huyo wa mapokezi alikwenda kuwagongea wateja wake bila kuwaeleza kama arobaini yao ilitimia.
Kwa mujibu wa mpelelezi aliyetumwa na mume wa mwanamke huyo, mwanamke ndiye aliyefungua mlango akiwa na taulo huku kamanda wake akiwa kitandani.
Shushushu huyo aliongeza kuwa, baada ya kushuhudia tukio hilo alipandwa na jazba na kutaka kuwapa kipondo lakini polisi walimzuia na kumtia pingu kamanda huyo hadi kituo cha polisi.

Kamanda huyo na askari wake walifikishwa kituoni hapo na kuchukuliwa maelezo ambapo mwanamke huyo aliweka wazi tangu bosi wake huyo alipompa ajira kwa sharti la kumpa burudani na mengineyo.
Kamanda Misana alifunguliwa kesi ya kudai rushwa ya ngono kwenye jalada lenye namba TBT/RB/2280/2014 na kutupwa rumande.