Blogger Widgets

May 23, 2014

Ikiwa Siku 2 Zimepita Tangu Msanii Adam Kuambiana Kufariki, Mchumba Wake Afungukna Na Kuweka Mahusino Ya Marehemu Na Msanii Wa Bongo Fleva


MAMBO yameanza! Siku mbili tu baada ya mazishi ya mwigizaji na mwongoza filamu mahiri Bongo, marehemu Adam Kuambiana, mrembo mmoja ameibuka na kusema alikuwa mchumba wa marehemu, Ijumaa linakujuza.


Mrembo anayejulikana kwa jina la Lulu Jumanne ‘Selina’.
Kwa mujibu wa mrembo huyo, Lulu Jumanne ‘Selina’, alifahamiana na marehemu Kuambiana mwaka 2006 akamwambia ndoa yake haipo sawasawa.


Alisema walianzisha uhusiano lakini haukuwa wazi katika jamii. Alisema siku moja akiwa anaishi Mwananyamala, wazazi wake walimtembelea.


“Nikiwa na wazazi nilimwona Kuambiana anapiga hodi, akaingia akiwa na  begi la nguo. Niliogopa kwani wazazi walikuwepo na walikuwa hawamtambui.


Lulu Jumanne ‘Selina’, akiwa na marehemu Kuambiana.

“Hata hivyo, walielewa yakapita, tukawa tunaishi wote nyumbani kwa kupika na kupakua,” alisema Selina ambaye naye ni mwigizaji.


Aliendelea kuweka wazi kwamba, baada ya hapo maisha yaliendelea lakini ikafika mahali marehemu akahamishia mapenzi kwa Mbongo Fleva, Stara Thomas yeye akawa ‘zilipendwa’.
Akizidi kuanika mambo kuwa mwaka jana Kuambiana alirudi kwake baada ya kutofautiana na Stara, akataka waendelee na mapenzi yao