
Hata yeye mwenyewe Shaa anatamani hilo litokee. “Supporting @vanessamdee #SwitchOn #WomenSupportingWomen #love #smile kama naona collabo vile….haha,” aliandika Shaa kwenye picha hiyo. Mashabiki wao nao wameona umuhimu wa waimbaji hao warembo kukutana kwenye wimbo mmoja.
“I real want to see you @vanessamdee and @shaa_tz to sing together ntafurahi sanaaaa nawapenda mnoooooo,” aliandika shabiki mmoja na mwingine kuandika”I called it first…best combo!!!!.” Naye muongozaji wa video nchini Adam Juma
akasema atapenda kuifanya video hiyo. “Positive people# would like to hear n shot that aisee @shaa_tz @vanessamdee,” aliandika.
Kama ikitokea, collabo hiyo inaweza kuwa ya hatari kuwahi kufanywa na wasanii wa kike. Vanessa Mdee ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania waliopo kwenye Kili Music Tour 2014.
No comments:
Post a Comment