Blogger Widgets

May 6, 2014

MFANO WAKUIGWA:Picha Mbalimbali zikionesha Nisha Akitoa Misaada Mbalimbali Kwa Watoto Yatima Huko Vingunguti.

Nisha akiwa na watoto hao
Star mkubwa wa filamu nchini Tanzania Salma Jabu Nisha ambaye filamu yake mpya ya ZENA na BETINA inatarajiwa kuingia sokoni tarehe 29 mwezi huu wa tano 2014 jana Jumapili alienda kutoa misaada katika kituo cha watoto yatima kilichopo vingunguti, Dar salaam. Nisha aliongozana na star mwenzake wa filamu ambaye pia ni rafiki yake wa karibu Happy Nyatawe huku Swahiliworldplanet ikishughudia tukio hilo la kuisaidia jamii. Nisha alitoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile unga wa kupikia, ndoo za mafuta, sabuni, juice na vitu vingine vingi. Baada ya hapo Nisha, Team Nisha, watoto hao yatima na walezi wao walijumuika kutoa burudani huku watoto hao baadhi wakionyesha vipaji vyao ikiwemo kucheza muziki na kuigiza. Nisha pia alitoa pesa taslim kwa mlezi wa kituo hicho ambaye hakusita kutoa shukrani kwa Nisha na team yake nzima kwa msaada huo. Angalia baadhi ya picha za tukio hilo...........
Nisha na Team Nisha wakiwasili kituoni hapo
Nisha akigawa juice kwa watoto
Baadhi ya misaada iliyotolewa
Happy Nyatawe akiwa karibu na Team Nisha
Nisha akiwa na mlezi wa kituo hicho