Blogger Widgets

May 22, 2014

Naomba Leo Niwasilishe Hii Taarifa Yenye Ukweli Kutoka kwa MamuAfrica Ni Jinsi Msanii Stara Thomas Akikiri ni Kweli Alikuwa Na Mahusisano na Marehemu Kambiana Wakati Marehemu Akiwa na Mke Wake ILA.....

 
Msanii Stara Thomas amefunguka kuhusiana na mahusino yake na aliyekuwa msanii wa bongo movie Adam Kuambiana aliyefariki wikiendi iliyopita na kuzikwa jana kwenye makaburi ya Kinondoni.
Stara amesema ni kweli aliwahi kuwa na mahusiano na Kuambiana lakini hata hivyo walitengena kutokana na kupishana baadhi ya tabia.

Anasema mahusiano yao yalianza walipokutana uwanja wa Taifa kwenye moja ya mechi iliyozikutanisha Bongo movie na Bongo flava na katika mahusinao yao hakuwahi kumwambia kama ana mke Zaidi ya kumwambia kuwa amewahi kuoa na ameachana na mke wake kwa talaka.

“Ni kweli nimewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Adam,uhusiano ambao ulifika mbali kiasi cha kutambuliwa nyumbani kwao kwa baadhi ya ndugu wakiwemo dada zake na hata babu yake mkubwa lakini hatukuweza kufikia kufunga ndoa kama tulivyokuwa tunafikiria,nakumbuka nilimuuliza kama ana mke akaniambia aliwahi kuoa na ameachana na mke wake”alisema Stara.


 

Amesema moja ya mambo makubwa ambayo walitofautiana ni pamoja na hasira kali kiasi cha kupelekea ugomvi mara kwa mara ,uvutaji wa sigara kupita kiasi wa Kuambiana ambaye hata alipokuwa akimueleza hakuwa akimuelewa,lakini pia kuna hitilafu ziliwahi kutokea kati yao walipokuwa safarini Zanzibar na Morogoro na mwisho akaona hawawezi kuishi kama mke na mume na kuamua kusitisha mahusiano.
 

“Unajua Adam alikuwa na kisukari sasa kwa kiasi kikubwa alikuwa anavuta sigara anapokuwa na stress zake na pia alikuwa mtu wa hasira sana,lakini kikubwa ni kutofautiana kwa baadhi ya tabia ambazo nikaona hatuwezi kuendelea na mahusiano yetu nikasitisha rasmi japo yeye mwenyewe aliomba kuwa atajirekebisha lakini ni vitu ambavyo vilikuwa vinajirudia nikaona hapana”Stara alisema.
Hata hivyo Stara amesema mbali ya kuwa na tofauti lakini Kuambiana hakuwa muhuni wa kubadili wanawake alikuwa ni mwenye kujiheshimu kwa kiasi kikubwa.Akizungumzia kuhusu fedha zinazodaiwa alikuwa nazo Kuambiana na kuibiwa,alisema hakuna kitu kama hicho kwakuwa fedha walizopeana siku ya mwisho kabla ya umauti kumkuta ilikuwa ni dola 100 ambazo washiriki wote wa filamu waliyokuwa wakiitengeneza walipatiwa.
Amesema mweka hazina wa kampuni ana hesabu zote ambazo zinahusiana na filamu hiyo pamoja na kiasi kilichotumika kwenye baadhi ya mambo yaliyohusiana na msiba na kutoka katika fedha hiyo wametoa fedha kiasi cha shilingi milioni 1 hapo jana wakati wa maziko ya msanii huyo.

Akifafanua Zaidi kuhusu filamu hiyo amesema filamu ina kisa cha kweli na wataingiza kisa kingine cha kweli cha kufariki kwa Kuambiana huku akisisitiza malipo ya filamu hiyo yatatoka kama ilivyo kwenye mkataba unaosema Kuambiana atalipwa nusu ya fedha ya filamu hiyo na nusu nyingine itaingia kwenye kampuni ambapo pia washiriki wataliopwa chao kama makubaliano yalivyo na mkataba upo.