Blogger Widgets

May 23, 2014

Pata Tarifa Kamili Juu ya Kuwasili Ndani ya Jiji la Dar Es Salaam Mchekeshaji wa Uganda, Kansiime Anne

Mchekeshaji wa kike maarufu wa nchini Uganda, Kansiime Anne anatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam August 2, mwaka huu.
10264317_10203091873331124_6823110432661911219_n
Kansiime atakuja kwa mwaliko wa Radio 5 itakayofanya uzinduzi rasmi wa masafa yake ya Dar es Salaam.
“Habari Tanzania! We are delighted to announce that Kansiime Anne has received and accepted the invitation to host the Launch of Radio 5 Tanzania’s new FM Frequency in Dar es Salam, Tanzania on August 02, 2014. While this will be Anne’s first visit to TZ, it may also be restricted due to the nature of the event, so please get in touch with Radio 5FM for details,” yamesema maelezo.

Kansiime alijipatia umaarufu kupitia mtandao wa Youtube na sasa amekuwa mchekeshaji wa Uganda anayetafutwa zaidi huku akiwa na show yake kwenye kituo cha runinga cha Citizen TV cha Kenya, iitwayo ‘Don’t Mess With Kansiime.