Blogger Widgets

May 21, 2014

Soma Alichokizungumza Penny Kuhususiana na Huyu Jamaa Anayesadikiwa kuwa ni Boyfriend wake

Baada ya kuachana na Diamond Platnumz, Peniel Mwingila aka Vj Penny ameendelea mbele na maisha yake, lakini amekanusha kuwa na mpenzi mpya kama ambavyo wengi wamekuwa wakidhani hasa wanapomuona yuko karibu na mwanaume mwingine.
Penny2
Leo Penny ameamua kuvunja ukimya wake na kukanusha habari zilizoenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa ana mpenzi mpya aitwaye Rummy, hiki ndicho alichokiandika:
Penny

“Ah come on people!!?? Kweli mi ni mkimya ila sasa mnavuka mipaka, seriously?? Am so disappointed to see posts that Rummy is my new boyfriend..mnatoa wapi hizi rumours? Just because sijibu shutuma natupiwaga haimanishi mimi sio binadamu kila siku mnanizushia mapya its not funny maisha yangu kutwa mnayafanya uwanja wa kutunga kitu, yes mnatukana na hakuna tusi jipya nawaacha ili mjifurahishe but now u r crossing the line, I have alot of respect for Rummy he is my homeboy na marafiki pia wa kiume nisiwe nao? Wengi wanajua rummy ni nani yangu ila making these stories aint cool at all. Enough has a limit! Nitukaneni all u want ila msinisingizie vitu sijafanya its just not fair at all. Kama new boyfriend ntaweka mwenyewe mapenzi hayajifichi ila tusizushiane uongo, nayavumilia mengi ila hili too much.”