AMINI NA LINAH |
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya bongo, Amini Mwinyimkuu ‘Amini’, imedai kuwa
anatarajia kutoa ngoma mpya ambayo atamshirikisha mpenzi wake wa zamani
Linah, ingawa bado ngoma haijaipa jina.
Amini
na Linah walikuwa wapenzi walioshibana lakini walikuja kuachana kwa
amani na upendo, na sababu kubwa za kutengana kwao hakuna anayejua zaidi
ya wao wenyewe.
Amini
ambaye ambaye kwa sasa yuko bize na ngoma hiyo ili iwe ya kimataifa
zaidi, alidai kuwa kutoka na mawazo ya watu kuwa yenye ana chuki na
Linah, sasa ameamua kumshirikisha katika ngoma yake ili kuweka wazi na
kufuta kauli za watu wenye nia mbaya.
Wakati
huo huo Linah naye alidai kuwa ameamua kufanya ngoma moja na Amini,
kwani wao ni wasanii na wanahaki ya kushirikiana ingawa anaamini kuwa
kuna watu baadhi ambao wanaamini wao bado ni wapenzi wakati ishu hiyo
yamesha isha zamani.
No comments:
Post a Comment