Blogger Widgets

September 12, 2013

Check Picha Mbali Mbali za Mwanamke aliyekamatwa Uwanja wa Ndege Akiwa na Mimba Bandia Iliyokuwa Ndani yake na Madawa ya Kulevya


Kila kukicha vita dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya inazidi kupamba moto, wakati mataifa mbalimbali yakizidi kuimarisha udhibiti wa biashara hiyo, na wafanyabiashara hiyo wanazidi kuja na mbinu mpya za kusafirisha dawa hizo.

mimba bandia

Huko Colombia mwanamke mmoja raia wa Canada amekamatwa uwanja wa ndege akiwa na tumbo la ujauzito wa bandia ambalo ndani yake alificha kilo mbili za dawa za kulevya aina ya Cocaine.

mimba-2

Polisi wa uwanja wa ndege wa Bogota Colombia alimshtukia mwanamke huyo raia wa canada Tabitha Leah Ritchie aliyeonekana kuwa na tumbo lisilo la kawaida ndipo baada ya kumkagua wakakutana na dawa hizo.