Blogger Widgets

October 29, 2013

Bongo Kama Mbele Siku Hizi:Wakati Mtoto wa Mabeste "Kendrick"Hajafikisha Hata Mwaka Mmoja Toka Azaliwe Apata Ngekewa ya kusainishwa ‘deal’ la kutangaza maduka ya ‘Pampers’

Mtoto wa rapper Mabeste, Kendrick ambaye ana miezi mitatu sasa, ataanza kuonekana akipitangaza maduka yanayouza ‘diapers’ maarufu kama Pampers, thanks kwa jitihada za baba yake.
941491_500655610033697_303479977_n
Kendrick

Akiongea na Bongo5, Mabeste amesema tayari amemfungulia mwanae akaunti kwenye mitandao ya kijamii ambako huko ndiko atakuwa akipromote maduka hayo.
“Mwezi ujao tu anaweza akaanza sababu nimemtengenezea page yake na blog yake ndio inakuja ambayo itakuwa inatangaza biashara kupitia social networks. Yale maduka yatakuwa yanamlipa mwisho wa mwezi,” alisema.
Mabesete

Mabeste

Katika hatua nyingine, Mabeste amesema amemfungulia mwanae email ambayo huweka picha zake kila siku akimpiga.
“Toka day one mama yake akiwa na ujauzito, nilikuwa nampiga picha hadi amejifungua, akikua ntampatia password na story ya maisha yake yote anakuja kuikuta kule.”