Blogger Widgets

May 24, 2014

Hebu Pata Muda wa Kujua Chanzo Chanzo cha Ugomvi Kati ya T.I.D na Dully Sykes Mpaka Kufikia Hatua ya Kurushiana Maneno

  

TID na Dully Sykes hawakai tena zizi moja. Wasanii hao wakongwe wanadaiwa kuzinguana baada ya Dully Sykes kutimiza miaka 15 nakudai kuwa kitu anachojivunia nikumfunika TID kwenye show iliyofanyika mwaka 2002 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee walipokuwa wakizindua album zao.
page

Kauli hiyo haikumpendeza TID aliyeamua kujibu kwa kusema: TID unaweza kumfunika mzee Mnyama wewe? Alivaa nguo zake za Kariakoo, kama mapazia hivi,unafikiri Dully Sykes anaweza akanifunika mimi? Nimesoma shule za kishua, nimefanya muziki kwa intelligence, hao watu wa Kariakoo washamba.”
Akiongea na 255 ya XXL, Clouds FM jana, Dully alijibu kauli hiyo ya TID na kusema: Ngoja nikwambie kitu kimoja TiD mimi nimempita miaka mingi, nimempita kila kitu yeye kanipita kasoma ndo alichonipita TID. Mimi kipindi hicho ndiye nimemkaribisha kwenye industry ‘mimi ndio Dully Sykes nipo juu mwaka 2002′, miaka mitatu nyuma mimi ndio nimetoka TID anatoka ndio nimemkaribisha. Halafu uzinguzi wetu TID alikuwa amelipa kosta mbili pale Magomeni akawaahidi atawapa hela wakifika pale Diamond round ya pili hajawapa hela ikabidi wale aliyowaleta kosta mbili wamzomee yeye, ushaelewaee kwahiyo TID kaamua kuongea uongo. Halafu TID ni mdogo wangu anajua mimi ni kaka yake, historia ipo na picha ninazo. Mimi ndio nilipendeza kushinda TID. TID alikuja kama mgambo pale alikuja kama mgambo na nguo za mgambo nikisema mwanajeshi atakuwa juu kidogo. Mimi na miaka mitatu nyuma TID ndo anatoka 2002 na Zeze. Rafiki yangu kusoma hujui hata hata picha pia, inaeleweka na inajulikana kijana wangu mdogo ndio hivyo.”
Kwa wale ambao hawaifahamu show hii, haya ni maelezo yaliyoandikwa mwaka 2002 kwenye mtandao wa African Hip Hop na mtu aliyehudhuria show hiyo.
Oya masela wangu nimeona niwadokezeeni kidogo yaliyojiri katika utambulisho wa albamu ya Dully Sykes na TID pale Diamond Jubilee.
Naweza kusema kwa asilimia mia onyesho lilifana kwani watu walizikonga nyoyo zao vilivyo kwa kupata ile kitu roho inapenda.
Kwa upande wa wasanii walioanza kupanda jukwaani walikuwa ni Mamnduli Mobb hawa si wengine ni MH.Temba na mwenzake Daz P a.k.a. Bwana Mkubwa na walianza na Track yao ya MASKINI JEURI TUMESHADATA TUMECHOKA NA NDOTO ZETU ZA ALINACHA,Baada ya hapo wakashusha KAMA UNATAKA KUJA HOME,SISTA DU UNATAKA KUJA HOME,Ilikuwa ni raha tupu kwani sista du aliyeimba chorus alikuwa ni mwakilishi tosha wa sista du anayeongelewa kwenye wimbo huo na haswa sehemu amayosema “jeans underwear inabana sista du utaweza kuinama” baada ya hapo wakamalizia na MPENZI NAKUMAINDI UWE WANGU MAANANI WACHA WAPIGE KELELE WANGA WAKICHOKA WENYEWE WABWAGE MANYANGA yaani hapo ilikuwa ni kelele toka kwa mashabiki huku wakiimba chorus sambamba nao kwa kweli naweza kusema jamaa waliwateka mashabiki kwa kiasi kikubwa.
Baada ya Manduli mobb akapanda PIG BLACK na wimbo wake NINI MNATAKA MAZEE Pig Black aliweza kuwachengua kutokana na Squad aliyopanda nayo ilikuwa ya watu kama kumi alafu wanaruka ruka kiutamu jukwaani wakidansi sambamba na beat si unajua sctrach za P-FUNK kwenye huo wimbo zinavyopendeza
Walipanda wasanii wengi siku hiyo ila turudi kwa wahusika wenyewe.
Alikuwa ni TID ndo alianza kupanda jukwaani na aliimba Takriban nyimbo nne kila nyimbo alipanda na show yake na mavazi tofauti.
Ikafuata zamu ya Dully nae aliimba nyimbo nne za kuanzia na sehemu ya kwanza hakuwa na show.
Ikaja zamu ya wasanii waalikwa na Alikuwepo MC NAPO alipanda na nyimbo kama “Fagio laChuma” pamoja na “Superstar wabongo”
Univesity corner hawakuwa nyuma kwani walipanda na wimbo wa MSINICHEKE na waliweza kukubalika ipaswavyo kwani baada ya show walipigiwa makofi.
Mwokozi wa mitaa ya kati nae alikuwa ndani ya nyumba huyu si mwingine ni IMAM ABAS na alipanda na wimbo MITAA YA KATI au
Kwa upande Msanii aliyeweza kuwapagawisha mashabiki kwa wimbo sambamba na dance alikuwa ni MIKE T kwani alionyesha kuwa alikuwa amejiandaa ipaswavyo na alianza na wimbo wa “KAMA NINGEKUWA STAR”
na kumalizia na “NAMPENDA”ambapo ndo aliwamaliza watu kwa kudance vizuri huku watu wote ndani ya nyumba wakiimba chorus “nampenda nasifa nakupa”
Kukosekana kwa Juma nature siku hiyo iliwakosesha watu wengi uhondo kwani nyimbo nyingi zilizoimbwa zilikuwa zinamshirikisha yeye kuanzia Manduli mobb “MASKINI JEURI”alioshirikishwa kwenye chorus,Imam Abas MITAA YA KATI alioshirikishwa chorus,MIKE T “nampenda” aloshirikishwa kwenye chorus na mwisho ni mabaga fresh walimkosa kwenye MTULIZE.
Mabaga waliweza kuwasuhusa watu kwa nyimbo mbili ya MTULIZE na TUNATAABIKA ambapo kwa back stage yao alikuwepo FANANI akiwapa kampani.
Wangine walioteka mashabiki lilikuwa ni kundi la gangwe MObb ambao walipanda stagini mara mbili awamu ya kwanza waliimba Mtoto wa Geti kali,na NJE NDANI na awamu ya pili waliimba RAP KATUNI na ASALI WA MOYO,mwingine aliyechengua alikuwa ni Q_CHIEF aliweza kuimba wimbo wake wa aseme na alikuwa amejiandaa vya kutosha kwani aliweza kufanya makeke ambapo wakati amemaliza beti ya kwaza wimbo ulistop na baragumu likalia akatokea mtu akaja pembeni yake akamrusha njiwa akiashiria versse yake ya pili anayosema “malaika nawatuma mwambieni nampenda”hii inaonyesha jinsi gani alikuwa amejiandaa.
Ikafuata awamu ya pili ya wahusika na alianza safari hii alikuwa Dully Sykes na hadi muda huo dully alikuwa amefunikwa kwani TID alikuwa mahiri kwenye show yake pamoja dance,Dully alianza a Salome na safarii alikuwa na show, ilikuwa ni show kali sijapata kuona kwani ilipigwa beat tupu na yeye pamoja na wacheza show wake waliweza kumudu beat na kucheza nalo sambamba ilikuwa ni makele na vifijo vilivyolipuka na hatimae akaaunganisha salome yenyewe yaani nyie wacheni baada ya kumaliza wimbo wa salome washabiki walipiga makelele wakiashiria tena yaani arudie wimbo wa Salome na Bila kukataa alianza tena show yak


e iliyokuwa kali kupita kiasi,baada ya salome aliimba Nyambizi,MONALISA na julieta
Ikafuata zamu ya TID nae alimalizia na nyimbo zake nne za mwisho na wa mwiso ulikuwa ZEZE ,Ingawa jay mo hakuwepo jukwaani lakini aliweza kuchana mwenyewe na dance yake yanguvu iliyowafanya watu wasielewe waende upande upi Dully au TID kwa upande wangu minasema wote walikuwa wamejiandaa vya kutosha na ndio maana nasema wote walingara
Je nyinyi wengine mliokuwepo mnasemaje nani alingara na nani alifunikwa?

No comments:

Post a Comment