Blogger Widgets

June 2, 2014

Soma Kinachoendelea Juu ya Tuhuma ya Mume wa Flora Mbasha Kutoonekanan Mpaka Sasa

TAHADHARI! Wakati akiwa hajulikani alipo huku akishtakiwa kwa tuhuma ya ubakaji wa shemejiye, jeshi la polisi Bongo limemtaka mume wa mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha kujisalimisha mwenyewe.
TAHADHARI! Wakati akiwa hajulikani alipo huku akishtakiwa kwa tuhuma ya ubakaji wa shemejiye, jeshi la polisi Bongo limemtaka mume wa mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha kujisalimisha mwenyewe.

 
Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, akiwa na mume wake, Emmanuel Mbasha.
Habari za ndani zilieleza kuwa polisi wa Kituo cha Tabata-Shule, Dar ndiyo wamemtaka kujisalimisha baada ya binti anayedaiwa kubakwa kufungua jalada kituoni hapo lenye namba TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi namba TBT/IR/1865/2014 akidai kutendewa unyama huo kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili wiki mbili zilizopita).
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho ndani ya jeshi hilo, zoezi la kumsaka limeanza tangu Mei 19, mwaka huu aliposhitakiwa na shemejiye kituoni hapo lakini hadi gazeti hili linakwenda mitamboni Jumamosi jioni, jitihada zilikuwa hazijazaa matunda.
 
Ilisemekana kwamba licha ya kuweka mikakati kabambe ya kumtia nguvuni ili ahojiwe kuhusiana na tuhuma hizo huku jeshi hilo likimtaka Mbasha kujitokeza kabla nguvu nyingi hazijatumika.
“Tunamtaka ajitokeze mwenyewe kabla hatujatumia nguvu nyingi kumsaka, maana jeshi lina mkono mrefu hivyo hana ujanja na ukizingatia yeye ni mtu maarufu,” kilisema chanzo.
Ilidaiwa kuwa, Mbasha alitoweka nyumbani kwake, Tabata-Kimanga wakati ambao mkewe (Flora) alikuwa amehamia hotelini kutokana na ugomvi mzito waliokuwanao.
Taarifa zaidi zilisema, kwa kuwa mlalamikaji alifikisha malalamiko hayo polisi akiwa na viambatanisho vya vipimo vya daktari vilivyoonesha kuingiliwa kimwili kwa nguvu, Mbasha anatakiwa ajitokeze ili kutoa maelezo ya upande wake na taratibu za kisheria ziendelee.
Jitihada za kumpata Mbasha zilishindikana kwa kuwa simu yake haipo hewani kwa siku kadhaa sasa.