Blogger Widgets

November 23, 2012

Shilole na Polisi wakiwa wanawasiwasi gari lake kuwa na Mzigo wa Bhangi.Walichokikuta sasa


MSANII wa anayefanya vizuri kwenye muziki na filamu Shilole, amenusurika kumakatwa na polisi baada ya kuhisiwa kuwa na misokoto ya bangi ndani ya gari lake na kusababisha kuhojiwa kwa dakika kadhaa maeneo ya Kinondoni.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo msanii huyo inadaiwa alikuwa akitokea kwenye ishu zake ndipo maafande hao wanaliokuwa wakitokea kwenye malindo yao walipomdaka na kumpeleka pembeni kwa lengo la kufanya upekuzi kwenye gari yake.


Inadaiwa kuwa polisi hao hawakukuta kitu chochote zaidi ya sigara za mpenzi wake, ambaye walikuwa wote usiku huo na hata hivyo hawakuwa na dalili zozote za kuwa wamelewa.


Shilole
alipozungumza na mwandishi wa DarTalk alidai kuwa tukio hilo lilimshangaza sana kwani hakuwa na bangi ndani ya gari lake na hajawahi kutumia kitu hiyo lakini polisi hao walimuhoji kana kwamba anatumia bangi.

Alidai kuwa kuna baadhi ya watu walitaka kumfanyia mchezo mchafu lakini walishindwa kwani alikuwa makini katika kila jambo ambalo alikuwa akilifanya usiku huo, na alipoulizwa kuwa usiku huo alikuwa anatoka wapi alidai kuwa katika harakati zake za hapa na pale.