Blogger Widgets

May 31, 2013

Ratiba Mpya Kabisa Iliyobadilika Muda Huu Kwa Kupokea Mwili Wa Marehemu Albert Mangwea.KESHO NDIO MWILI UNAFIKA


RATIBA YA MSIBA WA ALBERT MANGWEHA

Tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa watanzania wenzetu kwa ushirikiano wenu katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa ndugu yetu Albert Mangweha kilichotokea Afrika Kusini.
- Katika kufanikisha msiba na mazishi ya ndugu yetu mpendwa tunapenda kuchukua nafasi hii kukaribisha wizara husika, mashirika, makampuni na watu binafsi kutoa michango yenu kupitia mitandao ya simu zifuatazo :
- Kwa watumiaji wa mtandao Tigo, Nenda kwenye kutoa pesa toa kiasi unachotaka kuchangia , kisha andika namba ya wakala 00001 ,ambapo litatokea jina la Mangwair Contribution hapo utakuwa tayari umechangia.

-Tigo: Namna ya kuchangia, Nenda kwenye kutoa pesa , andika namba ya wakala ambayo ni 00001, chagua kiasi unachotaka kuchangia, Jina litakalokuja ni Mangwair Contribution baada ya hapo utakuwa umechangia.
-
Mpesa – 0754-967738

Pia kwa kutumia akaunti ya benki ifuatayo:
- Jina la Akaunti : Kenneth B. Mangweha
Nambari ya Akaunti: 2012505840
Benki : NMB
Pia kwa niaba ya kamati tunapenda kutoa ratiba kama ifuatavyo:
- Mwili wa marehemu utafika siku ya jumamosi tarehe 01/06/2013 saa 8 adhuhuri katika kiwanja cha Jk Nyerere na kupelekwa hospitali ya Muhimbili.
- SIku ya Jumapili tarehe 02/06/2013, tunapenda kuwakaribisha watanzania wenzetu katika viwanja vya Leaders kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu. Shughuli itakayoanza saa 2 ya asubuhi mpaka saa 6 mchana.
- Saa 6 mchana Mwili wa marehemu utaondoka kuelekea morogoro kwa ajili ya maziko yatayofanyika siku ya jumatatu.
- Siku ya jumatatu tarehe 03/06/2013, mwili ya marehemu utafika saa 4 asubuhi nyumbani kwa mama yake maeneo ya Kihonda mjini Morogoro saa sita kutakuwa na chakula na baada ya hapo tutaaga mwili wa marehemu kwa ajili ya Maziko .
Tukiamini kila mwenye uwezo atachangia katika kufanikisha shughuli hii tunatanguliza shukurani zetu za dhati.
Pia tunaomba watanzania mujitokeze kwa wingi katika kuaga mwili wa marehemu katika kuonyesha upendo wetu kwa ndugu yetu Albert Mangweha.
Lakini Usiku Huu wa Tarehe 31.05.2013 Ndani EATV FNL Mchizi Mox  Wametoa Report kuwa Mwili Utafika Jumapili Bado Wanachanganya