Blogger Widgets

December 18, 2013

Shuhudia Picha Jinsi Makahaba wa Kenya walivyofanya Maandamano Kuitaka Serikali Yao Idhinishe UKAHABA

MAKAHABA KENYA WAFANYA MAANDAMANO KUITAKA SERIKALI YAO IDHINISHE UKAHABA Makahaba mjini Nairobi Kenya waliungana na wenzao duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga unyanyasaji dhidi yao.
Waliandamana Jumanne kulalamikia kile wanachosema ni unyanyasaji wanaofanyiwa na polisi pamoja na askari wa baraza la jiji wakati wakiendesha biashara zao.

Walikusanyika katikati ya mji na kuelekea katika ofisi za baraza la jiji kuwasilisha malalamiko yao wakisema kuwa wamechoka kuhangaishwa na polisi na wanataka ulinzi.

Mwanaharakati wa maswala ya biashara ya ngono, John Mathenge aliyekuwa miongoni mwa waandamanaji, alisema kuwa wengi wao wameuawa na kunyanyaswa hata na wateja wao pamoja na maafisa wa usalama.


Siku hii ya kimataifa, huadhimishwa kila mwaka tarehe 17.
Biashara ya ngono imeharamishwa nchini Kenya lakini baadhi ya watetezi wa makahaba wanasema kuwa katiba haijaeleza bayana ikiwa mtu atakayekamatwa akijihusisha na biashara hiyo achukuliwe hatua gani za kisheria.
Mathenge alielezea kuwa lazima watu wakome kuwabagua wanaofanya biashara ya ngono, kwani ni kazi kama kazi nyingine tu.
Wengi walilalamika kuwa jamii imepuuza watu wanaofanya biashara ya ngono wala haiwatetei wakati wanaponyanyaswa au kuuawa .
Ripoyi iliyotolewa mwaka jana kuhusu makahaba mjini Nairobi ilisema kuwa wanahangaiswa sana na askari wa baraza la jiji na kuwa wengi wao huachiliwa tu pindi wanapotoa rushwa.

No comments:

Post a Comment